Nijuze Habari

Rais Samia afanya uteuzi

Filed in New by on 12/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

Rais Samia Suluhu Hassa amemteua Balozi Ali Siwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

Uteuzi huo umefanyika jana Jumamosi December 11, 2021 ambapo Balozi Siwa ameteuliwa kwa kipindi cha pili kushika nafasi hiyo kutokana na muda wa bodi hiyo kuisha September 21 mwaka huu.

Aidha Rais Samia pia amewapangia vituo vya kazi mabalozi wanne, ambapo Balozi Said Mussa amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Kuwait, Balozi Fredrick Kibuta amekuwa Balozi wa Tanzania nchini Urusi.

Wengine ni Balozi Said Mshana ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) huku Balozi Alex Kalua akiteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania katika Taifa la Israel.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.