Nijuze Habari

Rais Samia afanya uteuzi mpya

Filed in New by on 27/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

Rais Samia Suluhu Hassan, amemteua Jaji Jackob Mwambegele kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), akichukua nafasi ya Jaji Semistocles Kaijage ambaye amemaliza muda wake.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Jaffar Haniu inaeleza kuwa uteuzi huo pamoja na teuzi nyingine nne alizozifanya Rais Samia umeanza December 23, 2021 ambapo kabla ya uteuzi huo, Jaji Mwambegele alikuwa Mjumbe wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Katika hatua nyingine, Rais Samia amemteua Jaji Mwanaisha Kwariko kuwa mjumbe wa NEC akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Mwambegele ambapo pia amemteua Jaji Sam Mpaya Rumanyika kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambapo kabla ya uteuzi huo, alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu.

Katika uteuzi mwingine, Rais Samia amewateua Profesa Khamis Dihenga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB), akichukua nafasi ya Profesa William Anangisye ambaye amemaliza muda wake na Dk. Musa Kissaka aliyeteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Serikali Mtandao.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.