Nijuze Habari

RAIS Samia afanya uteuzi mpya UDSM

Filed in Michezo by on 25/08/2022 0 Comments

RAIS Samia afanya Uteuzi mpyaRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi kama ifuatavyo:

Nijuze Habari Application

RAIS Samia afanya uteuzi mpya UDSM

RAIS Samia afanya Uteuzi mpyaRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa Wenyeviti wa Bodi kama ifuatavyo:

Rais amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Balozi Maajar anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu, Mhe. Damian Lubuva ambaye alimaliza muda wake.

Rais Samia pia amemteua Prof. William Andey Lazaro Anangisye, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA). Prof. Anangisye anaendelea kwa kipindi cha pili.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Alhamisi August 25, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.Zuhura Yunus ambapo ameeleza kuwa uteuzi huo unaanza Agosti 23, 2022.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.