RAIS Samia anunua magoli ya Tanzania vs Uganda 28 March 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


RAIS Samia anunua magoli ya Tanzania vs Uganda 28 March 2023

RAIS Samia anunua magoli ya Tanzania vs Uganda 28 March 2023
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan aipongeza timu ya taifa ya Tanzania “Taifa Stars” kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda, mchezo wa Kundi F uliofanyika kwenye Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri jana Machi 24, 2023
Aidha, kuelekea mchezo wa marudiano utakaochezwa Jumanne ya Machi 28,2023 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Rais Samia ameahidi kutoa Shilingi Milioni 10 kwa kila bao litakalofungwa na Tanzania.
Bao pekee katika mchezo huo lilifungwa na Simon Msuva anayechezea soka la kulipwa katika klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia dakika ya 68 akimalizia krosi ya Dickson Job.
Ushindi huo unaifanya Taifa Stars ifikishe pointi nne na kusogea nafasi ya pili nyuma ya Algeria wenye pointi tisa, huku Uganda inayobaki na pointi yake moja ikiendelea kushika mkia nyuma ya Niger yenye pointi mbili baada ya timu zote kucheza mechi tatu.
Katika hatua nyingine, RAIS Samia Suluhu Hassan alinunua tiketi 2,000 kwaajili ya kampeni ya kuhamasisha Mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo wa Marudiano dhidi ya Uganda.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa pia naye ameshiriki katika Kampeni hiyo kwa kununua tiketi 2000 kwaajili ya mashabiki.
Wadau wengine walionunua tiketi kwaajili ya kampeni ya kuhamasisha Mashabiki kujitokeza kwa wingi kwenye mchezo huo wa Marudiano dhidi ya Uganda ni;
- Anthony Mtaka – Mkuu wa Mkoa wa Njombe (200)
- Anthony Mavunde – Naibu Waziri wa Kilimo – (200)
- Abdallah Mwaipaya – Mkuu wa Wilaya ya Mwanga (100)
- Murtaza Mangungu – Simba SC (600)
- Salim Abdallah Try Again – Simba SC (500)
- Sunderland (200)
- Online Media (100)
- Lampand Electronics (100)
- JSP Market Link (200)
- CRDB Bank (1,000)
- Lameck Nyambaya – Mwenyekiti DRFA (200)
- Alex Ngai – Intrev Limited (200)
- Eng. Hesri Said – Yanga SC (1,500)
- Swahili Water (100)
- Kitambaa Cheupe Sinza & Tabata (300)
- Silent Ocean & K4S (1,000)
- Abdulkarim Popat – Azam FC (1,000)
- Idd Azam (300)
- Bullet Force Security (1,00)
UNAWEZA PIA KUSOMA👇
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: RAIS Samia anunua magoli ya Tanzania vs Uganda 28 March 2023, Tanzania vs Uganda 28 March 2023, Tanzania vs Uganda head to head, Tanzania vs uganda prediction, Tanzania vs uganda results