RAIS Samia aongeza motisha Simba na Yanga Kufuzu Nusu Fainali CAF

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


RAIS Samia aongeza motisha Simba na Yanga Kufuzu Nusu Fainali CAF

RAIS Samia aongeza motisha Simba na Yanga Kufuzu Nusu Fainali CAF
Rais wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan ameongeza fedha za motisha kwa timu za Simba na Yanga kutoka shilingi milioni 5 hadi milioni 10 kwa kila goli endapo timu hizo zitafuzu kucheza Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
Kwa mujibu wa Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, magoli yatakayolipiwa motisha hiyo (shilingi milioni 10 kila goli) ni yale yatakayofungwa katika dakika 90 za mchezo au dakika 120 na sio magoli ya penati.
Rais Samia amezitakia kila la kheri timu hizo na amewataka Wachezaji kujituma Uwanjani na kutumia maarifa yao yote kuhakikisha wanashinda Michezo yao ya Robo Fainali ili wafanikiwe kuingia Nusu Fainali ambapo kila goli litakuwa shilingi Milioni 10.
Simba inacheza mchezo wa marudiano leo dhidi ya Wydad Casablanca nchini Morocco ikiwa na mtaji wa bao 1-0 ilioupata katika mchezo wa kwanza wakati Yanga itacheza mchezo wa marudiano Keshokutwa Jumapili dhidi ya Rivers United ikiwa na mtaji wa mabao 2-0 ilioupata ugenini nchini Nigeria.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: RAIS Samia aongeza motisha Simba na Yanga Kufuzu Nusu Fainali CAF