Nijuze Habari

RAIS Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa Mara

Filed in Habari by on 01/08/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

RAIS Samia atengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa Mara

SIKU tatu baada ya Dkt.Raphael Chegeni kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, uteuzi wake umetenguliwa usiku wa kuamkia Leo Jumatatu.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo July 31, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus ambayo imesema kuwa Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi huo na kumteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuchukua nafasi hiyo.
Rais Samia alimteua Dkt.Raphael Chegeni kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara July 28, 2022 kuchukua nafasi ya Ally Hapi.
Katika taarifa ya Ikulu imesema, mkuu huyo wa nchi amemtengua uteuzi wa Dkt.Chegeni huku nafasi hiyo ikichukuliwa na aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Magereza Tanzania, Meja Jenerali Suleiman Mzee.
 Meja Jenerali Suleiman Mzee
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Meja Jenerali Suleiman Mzee kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara na kutengua uteuzi wa Dkt.Raphael Masunga Chegeni,” imesema taarifa hiyo.
telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.