Nijuze Habari

RASMI Morrison arejea Yanga SC

Filed in Usajili by on 04/07/2022 0 Comments

Bernard Morrison arejea Yanga SCKLABU ya Young Africans SC imetangaza rasmi kumrejesha winga wake Mghana, Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 29 kutoka kwa watani zao Simba SC.

Nijuze Habari Application

RASMI Morrison arejea Yanga SC

Bernard Morrison arejea Yanga SCKLABU ya Young Africans SC imetangaza rasmi kumrejesha winga wake Mghana, Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 29 kutoka kwa watani zao Simba SC.

Hiyo ni baada ya sintofahamu ya miezi kadhaa baada ya kuachana na Simba SC na baadae kurejea nchini Tanzania na ujumbe maalum uliosomeka;

“Mara nyingi tunakatishwa tamaa na wale tunaowapenda na kuwaamini. lakini wacha nifanye hadithi yangu kuwa fupi na rahisi, nahitaji vipande 100 vya jezi za Simba kutoka kwa mashabiki waaminifu ili zipewe marafiki na familia nchini Ghana”Benard Morrison arejea Yanga SC

“Hii ni kutokana na nyinyi mashabiki kuniaga kwa sababu nitakatishwa tamaa ikiwa nitaendelea kusubiri kupata moja kutoka kwa klabu yangu. Tafadhali andika jina lako nyuma na namba 3. Anyone interested can bring to me at sea breeze mbezi beach and call me 0745460326. Nimefika Dar❤️ I WILL ALWAYS LOVE YOU ALL THOUGH.”

Aidha Morrison Katika mahojiano na Global TV Online alimuomba Rais Samia Suluhu Hassan kuruhusu kupata uraia wa Tanzania kutokana na mapenzi aliyonayo kwa nchi hii.

Morrison alisema hayo kupitia video iliyowekwa kwenye YouTube ya Global, huku akionekana anapiga magoti na kuomba msaada huo kwa Rais wa nchi Mama Samia Suluhu Hassan.

“Mama Samia naomba nipe passport ya Tanzania, naipenda sana Tanzania na hata kamasitocheza hapa lakini patakuwa nyumbani kwasababu naona kuna mapenzi, hii sehemu ni salama kwaiyo nataka kukaa hapa”. Alisema Morrison

Vilevile alisema kama atakubaliwa kuwa raia wa Tanzania yupo tayari kucheza timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Benard Morrison Yanga SCKatika mahojiano hayo Morrison aliweka wazi mambo mengi, ikiwemo sababu za kuondoka Simba SC

Morrison alisema “Walinipa mapumziko maana nilikataa kusaini mkataba mpya, kama ningecheza Simba miaka 5 au 10 halafu mwisho wa siku nikarudi Ghana sina hela au kumpigia mwenyekiti naomba hela kuisaidia familia yangu isingekuwa kitu kizuri.

“Niliomba mkataba mzuri, maboresho kwenye mkataba ili niwe vizuri kuihudumia klabu na haikufanyika hivyo, nilikuwa na kikao na Barbara na sababu ya hicho kikao ni kwa sababu tulicheza mechi dhidi ya Yanga na ile mechi nilipata majeraha na awali tayari nilikuwa majeruhi kwenye mechi dhidi ya Orlando Pirates.

“Baada ya mechi daktari hakunifuata kunihudumia wala kujua hali yangu, nilimtumia meseji nyingi kuwa sipo sawa lakini hakufanya hivyo, niliwaambia hamnijali hivyo nililazimika kujihudumia mwenyewe nikiwa nyumbani.

“CEO alinipigia simu nikaenda ofisini kwake akaniambia wachezaji wanahasira, wanasema hawataki niende tena kambini wala mazoezini, kocha analalamika siwaheshimu, hawataki niende mazoezini hivyo malalamiko ni mengi ni kwa nini nafanya hivyo?

“Nilimjibu sio kweli sidhani kama wachezaji wanaweza kufanya hivyo maana ndio haohao wachezaji wananipigia simu nisipoonekana kambini kunijulia hali lakini wewe CEO unasema hivi.

“Kocha alinipigia simu tukaongea kama dakika 40 nikamuuliza baada ya mkutano wangu na CEO unadhani kuna nini kitatokea akanijibu hadhani kama kuna namna ya mimi kurudi klabuni na kwa vile CEO aliniambia nenda ukakae nyumbani usubiri nitakupigia nikajua kuna jambo linaendelea.

“Asubuhi yake nilimpigia CEO akaniambia niende ofisini kwake, nilipoenda akaniambia mambo mawili, la kwanza nikubali kwenda nyumbani nikae nje ya klabu hadi mwisho wa msimu halafu watawaambia mashabiki nimeenda nyumbani kwa matatizo ya kifamilia na nitarudi mambo yakiwa sawa au ataweka kwenye social media kuwa wamenisimamisha hadi mwisho wa msimu,” amesema Morrison katika sehemu ya mahojiano hayo.

Aidha Klabu ya Simba SC ilitoa taarifa ya kuachana na Morrison kwenye mitandao yake ya kijami Ijumaa ya May 13,2022 kufuatia mkataba wake kufikia kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Taarifa ya Simba ilitaja sababu za kufanya hivyo kuwa ni kutaka kumpa muda wa kupumzika kiungo huyo hadi mwishoni mwa msimu huu, ili kutatua matatizo yake binafsi.

Taarifa hiyo ilisema kuwa  “Simba SC imefikia maamuzi haya baada ya pande zote mbili kukubaliana kwa lengo la kumpa nafasi Morrison kupumzika na kushughulikia mambo yake binfasi.”

“Tunatambua na kuthamini mchango wa Morrison katika miaka miwili aliyoitumikia klabu yetu na kuisaidia kupata mafanikio kadhaa ikiwemo kucheza Robo Fainali ya michuano ya Afrika Mara Mbili, Kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports na Ubingwa wa Kombe la Mapinduzi.” imeeleza sehemu ya barua ya klabu ya Simba SC.

Muda mchache baada ya Uongozi wa Simba SC kutangaza hadharani kumpa mapumziko hadi mwishoni mwa msimu huu, Kiungo Mshambuliaji wao Bernard Morrison naye aliandika;

SIMBA yaachana na Morrison, mwenyewe afunguka ukweli“Nina moyo mzito kutangaza kuwa sitakuwepo kwa muda uliosalia wa msimu huu kwa sababu ya masuala ya kifamilia ambayo ni nje ya uwezo wangu, na huenda yakaathiri utendaji wangu wa kazi ikiwa nitaendelea kuitumikia klabu”.

“Mengi yanahitajika kusemwa kuhusu hilo lakini naitakia klabu kila la kheri katika michezo yetu iliyosalia. Natumai na ninaomba nitatue hili haraka iwezekanavyo ili nijiunge na timu tena”.

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

DOWNLOAD APP MPYA YA NIJUZE HABARI BURE HAPA

UPATE KUTAZAMA MECHI LIVE, MAGAZETI YA KILA SIKU ASUBUHI PAMOJA NA HABARI NYINGINE NYINGI.

TEMBEA NA DUNIA MKONONI MWAKO UKIWA NA APP HII, FURAHIA HABARI NA MATUKIO KILA WAKATI.

Download Bure App mpya ya Nijuze Habari kuweza kuangalia Mpira na utaweza kuona matokeo na ratiba ligi zote kubwa Duniani.

APP HII PIA INAKUSOGEZEA

👉Habari za Kitaifa na kimataifa kutoka vyanzo mbalimbali ndani na nje ya Tanzania
👉Habari za Michezo na Usajili ndani na nje ya Tanzania
👉Breaking News
👉Elimu na Afya
👉Kutazama Mechi Mubashara za ndani na nje ya Tanzania
👉Taarifa ya Habari kila siku na Vipindi Mbalimbali kutoka Local Tvs
👉Kusikiliza Radio Online
👉Kucheck Movie kutoka (Maisha Magic Bongo na Maisha Magic East n.k)
👉Audio na Videos mpya kila siku
👉 Ajira mpya kila siku
👉Gospel na Makala mbalimbali.

BOFYA 👉👉👉 HAPA KUDOWNLOAD BURE

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.