Nijuze Habari

RASMI Simba kucheza na Mabingwa wa Ethiopia (Simba Day)

Filed in Michezo by on 05/08/2022 0 Comments

RASMI Simba kucheza na Mabingwa wa EthiopiaNI rasmi sasa mechi ya kirafiki ya Kimataifa kwenye kilele cha Tamasha la Simba Day litakalofanyika Jumatatu ya August 082022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam itakuwa ni Simba SC dhidi ya St. George kutoka Ethiopia.

Nijuze Habari Application

RASMI Simba kucheza na Mabingwa wa Ethiopia

St. George ni Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini humo wakiwa ndiyo Mabingwa waliotwaa Ubingwa mara nyingi zaidi wakifanya hivyo mara 29.

St. George wakiwa na Kikosi chao kamili watawasili nchini Jumamosi ya August 06 saa saba mchana ambapo watapata nafasi ya kufanya mazoezi Jumapili kabla ya mtanange siku ya kilele cha Simba Day Jumatatu.

RASMI Simba kucheza na Mabingwa wa Ethiopia

Aidha mchezo dhidi ya St. George utakuwa kipimo kizuri Simba SC baada ya mazoezi ya wiki tatu nchini Misri na itaipa dira kuelekea msimu mpya wa Ligi 2022/2023.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo Simba SC itawatambulisha wachezaji wapya na waliokuwepo kwaajili ya msimu huu wa 2022/2023 pamoja na benchi zima la Ufundi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.