Nijuze Habari

RASMI Simba yamtambulisha Kocha mpya, CV yake hii hapa

Filed in Usajili by on 28/06/2022 0 Comments

KLABU ya Simba SC rasmi imemtangaza kocha Zoran Manojlovic mwenye umri wa miaka 59 mwenye uraia pacha wa Serbian/Ureno kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam akisani mkataba wa mwaka mmoja kuirithi mikoba iliyoachwa wazi na Pablo Franco.

Nijuze Habari Application

RASMI Simba yamtambulisha Kocha mpya, CV yake hii hapa

KLABU ya Simba SC rasmi imemtangaza kocha Zoran Manojlovic mwenye umri wa miaka 59 mwenye uraia pacha wa Serbian/Ureno kuwa Kocha Mkuu wa Klabu hiyo yenye makazi yake mtaa wa Msimbazi Jijini Dar es salaam akisani mkataba wa mwaka mmoja kuirithi mikoba iliyoachwa wazi na Pablo Franco.

Zoran Manojlovic Simba SC

Klabu ya Simba imesema kuwa imejiridhisha juu ya ubora na uzoefu wa kocha Zoran hasa katika Soka la Afrika ambacho ndicho kigezo kikuu kilichozingatiwa katika kumuajiri.

Kabla ya kutua Simba SC, Kocha Zoran mwenye umri wa miaka 59 alikuwa anaifundisha Al Tai FC ya Saudi Arabia ambayo alijiunga nayo kutokea CR Belouizdad ya Algeria na kuiwezesha kufika robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.

Zoran Manojlovic Simba SCZoran pia amewahi kuifundisha miamba ya ya Soka Afrika Wydad Athletic Club ya Morocco, mwaka 2018 Zoran aliifikisha Primero De Agosto ya Angola Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika ikiwa ni mara ya kwanza katika historia ya Klabu hiyo.

Aidha Zoran si mgeni Tanzania kwani amewahi kuja Tanzania na timu ya Al Hilal ya Sudan kushiriki mashindano ya Super Cup yaliyoandaliwa na Klabu ya Simba SC mwaka jana.

Zoran Manojlovic Simba SCKlabu ya Simba SC imempa malengo ya kuhakikisha anaifikisha Klabu hiyo Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika (CAF Champions League) pamoja na kuurejesha Ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) na Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup).

Klabu ya Simba SC imesema kuwa kocha Zoran anatarajiwa kuanza kukitumikia kibarua chake mapema kwenye maandalizi ya msimu ujao wa 2022/2023 (Pre Season) ambayo itatangazwa hivi karibuni.

About Zoran Manojlović Simba New Coach  Zoran Manojlović (born 21 July 1962) is a Serbian football coach who was most recently the coach of Saudi Arabian club Al-Tai.

Manojlović began his coaching career in Portugal.

Manojlović coached three club sides in Angola,including Primeiro de Agosto (between December 2017 and July 2019) whom he guided to the African Champions League semi-final in 2018.He also served as an assistant coach at Kabuscorp in 2012.

Zoran Manojlović
Zoran Manojlović

Manojlović was appointed head coach of Moroccan club Wydad AC in July 2019. In November 2019 he said he was “thrilled” to be working at the club. He left the club in January 2020.

In October 2020 he became manager of Sudanese club Al-Hilal Club.

In April 2021 he became manager of Algerian club CR Belouizdad.

On 30 August 2021, Manojlović was appointed as the manager of Saudi Arabian club Al-Tai. On 4 November 2021, he was sacked with the club sitting at the bottom of the table.

Zoran Manojlović
Personal information
Date of birth 21 July 1962 (age 59)[1]
Teams managed
Years Team
2017–2019 Primeiro de Agosto
2019–2020 Wydad AC
2020–2021 Al-Hilal Club
2021 CR Belouizdad
2021 Al-Tai

 

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.