telegram Nijuze Habari

Ratiba ya Fainali AFCON 2021

Filed in Michezo by on 04/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

KIPA Gabaski ndiye aliyekuwa shujaa , baada ya kuokoa mikwaju miwili ya penati na kulisaidia Taifa lake la Misri kuwaondoa katika michuano hiyo wenyeji Cameroon kwenye mechi ilioamuliwa na mikwaju ya penalti kufuatia sare ya bila kwa bila ndani ya dakika 120.

Hatua hiyo sasa itazikutanisha Misri na Senegal katika Fainali ya Afcon 2021 Jumapili ya February 06,2022 saa 4:00 Usiku.

Fainali hiyo itawakutanisha washambuliaji wawili wa Klabu ya Liverpool Mohammed Salah dhidi ya Sadio Mane katika uwanja huo huo wa Olembe uliopo katika Mji Mkuu wa Younde nchini Cameroon.

Mechi hiyo iliojawa na ghadhabu katika dakika za lala salama ilimfanya Kocha wa Misri Carlos Quiroz kupigwa kadi nyekundu kwa kupinga maamuzi ya refa na wasaidizi wake kwa hasira.

Mbali na mechi hiyo kuwakutanisha washambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane, Fainali hiyo itakuwa ya kwanza katika Mechi tatu kati ya Misri na Senegal katika kipindi cha miezi miwili, kwa kuwa watalazimika kuamua mshindi atakayewakilisha Afrika katika kombe la Dunia nchini Qatar.

Wenyeji Cameroon wao watacheza na Burkina Faso Katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu Kesho Jumamosi February 05,2022.

Kulikuwa na maandalizi makali kabla ya mechi hiyo huku rais wa shirikisho la soka nchini Cameroon Samuel Etoo akiitaja mechi hiyo kuwa ‘vita’ katika hotuba yake.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *