Nijuze Habari

Ratiba ya Kombe la Mapinduzi 2022

Filed in Michezo by on 27/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA watetezi, Young Africans SC wamepangwa Kundi B katika michuano ya Kombe la Mapinduzi 2022 pamoja na wenyeji, Taifa Jang’ombe na KMKM zote za Zanzibar.

Washindi wa pili wa msimu uliopita, Simba SC wao wamepangwa Kundi C pamoja na wenyeji watupu pia, Sellem View na Mlandege FC.

Kundi A lenyewe lina timu mbili za kila upande, Azam FC na Namungo za Bara na Yosso Boys na Meli City za Zanzibar.

Michuano hiyo inatarajiwa kuanza Jumapili ya January 02, mwakani na Simba watacheza Januari 05 dhidi ya Sellem View, wakati Young Africans SC watamenyana na Taifa Jang’ombe siku hiyo hiyo  mechi zote zikipigwa Uwanja wa Amaan Mjini Zanzibar.

Nusu fainali ya mashindano hayo makongwe Visiwani Zanzibar itapigwa January 10 huku Fainali yake ikita­rajiwa kupigwa January 13,2022.

Makundi ya Mapinduzi Cup 2022.

Kundi A
Azam FC
Namungo FC
Yosso Boys
Meli 4 City

Kundi B
Young Africans SC
Taifa Jang’ombe
KMKM

Kundi C
Selem View
Simba SC
Mlandege

Hii hapa ratiba kamili ya Mapinduzi Cup 2022

➡️January 02,2022
17:15 Namungo FC vs Meli 4 City

➡️January 03,2022
16:15 Selem View vs Mlandege FC
20:15 Taifa Jang’ombe vs KMKM

➡️January 04,2022
16:15 Namungo FC vs Yosso Boys
20:15 Azam FC vs Meli 4 City

➡️January 05,2022
16:15 Simba SC vs Selem View
20:15 Young Africans SC vs Taifa Jang’ombe

➡️January 06,2022
16:15 Yosso Boys vs Meli 4 City
20:15 Azam FC vs Namungo FC

➡️January 07,2022
16:00 Young Africans SC vs KMKM
20:15 Simba SC vs Mlandege FC

➡️January 08,2021
16:15 Azam FC vs Yosso Boys

➡️January 10,2022 /Nusu Fainali
16:15 Mshindi wa 1 Group A vs Mshindi wa 1 Group B
20:15 Mshindi wa 2 Group A vs Mshindi wa kwanza Group C

➡️January 13,2022/Fainali
20:15 Mshindi wa Nusu Fainali ya kwanza vs Mshindi wa Nusu Fainali ya Pili.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.