Robertinho kuelekea mchezo vs Wydad Casablanca 28 April 2023

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


Robertinho kuelekea mchezo vs Wydad Casablanca 28 April 2023

Robertinho kuelekea mchezo vs Wydad Casablanca 28 April 2023
Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba Roberto Oliviera ‘Robertinho’ amesema kuwa kesho hawatacheza dhidi ya Wydad Casablanca kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa wiki iliyopita katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Robertinho amesema kuwa kesho watakuwa ugenini kwa hiyo wataingia na mbinu tofauti za kucheza aina hiyo mchezo haiwezi kuwa sawa na ile ya mkondo wa kwanza.
Robertinho ameongeza kuwa lengo la Simba litakuwa ni lile lile kucheza vizuri na kupata ushindi ili tufuzu hatua ya Nusu Fainali.
“Tumejiandaa na mbinu tofauti za kucheza mchezo wa kesho wa maruadiano wa Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad.
“Haiwezi kuwa sawa na vile tulivyocheza mechi ya kwanza ya nyumbani, nawaamini wachezaji wangu watafuata maelekezo tuliyowapa. Tumejipanga kucheza vizuri na kupata ushindi,” amesema Robertinho.
Kwa upande wake kiungo mshambuliaji, Pape Osmane Sakho amesema kuwa Wachezaji wako tayari kimwili na kiakili kupambana kuhakikisha tunatimiza malengo.
“Sisi wachezaji tupo tayari, tumepata maandalizi ya kutosha, tupo tayari kukamilisha kazi tuliyoianza wiki iliyopita tukiwa nyumbani,” amesema Sakho.
Kwa upande wa Kocha Msaidizi, Juma Mgunda, kuelekea mchezo wao wa ugenini dhidi ya Wydad Casablanca, amesema kuwa wachezaji wako vizuri na wanaitaka mechi, kilichobaki ni maombi na sala za Watanzania.
Download Video Juma Mgunda, kuelekea mchezo dhidi ya Wydad Casablanca
Donwload Video Robertinho kuelekea mchezo dhidi ya Wydad Casablanca
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.
Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA
Tags: Robertinho kuelekea mchezo vs Wydad Casablanca 28 April 2023