Nijuze Habari

Rungu la TFF lavikumba Vilabu, Wachezaji, Makocha, Mashabiki na Waamuzi

Filed in Michezo by on 28/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Rungu la TFF lavikumba Vilabu, Wachezaji, Makocha, Mashabiki na Waamuzi.

Kocha wa Klabu ya Simba SC, Pablo Franco ametozwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na wanahabari mara baada ya mchezo kati ya Mbeya City na Simba kumalizika

Pablo pia amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya sh. 500,000 (laki tano) kwa kosa kupiga teke chombo maalum cha kuhifadhia barafu/vinywaji vya baridi wakati mchezo wa Mtibwa Sugar na Simba SC.

Kocha huyo pia ametozwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na Wanahabari mara baada ya mchezo kati ya Mtibwa Sugar na Simba kumalizika.

Pablo pia ametozwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na Wanahabari mara baada ya mchezo wa Kagera Sugar na Simba SC kumalizika.

JINSI ya kushinda Mamilioni na ZEPPELIN SOKABET

Beki wa Klabu ya Young Africans SC, Djuma Shabani amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya sh. 1,000,000 (milioni moja) kwa kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania.

Mwamuzi wa kati Hance Mabena kutoka Tanga ameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitatu (3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri vema sheria za mpira wa miguu kwenye tukio la mchezaji Djuma Shabani.

Mwamuzi wa msaidizi namba moja, Paschal Joseph kutoka Shinyanga na mwamuzi wa akiba, Jackson Samwel wa Arusha wameondolewa kwenye ratiba ya waamuzi kwa mizunguko mitano (5) kwa kosa la kushindwa
kumsaidia mwamuzi wa kati, Hance Mabena katika kutafsiri vema sheria.

Maamuzi mengine ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (TPLB).

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.