Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

Filed in Michezo by on 13/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

KICHAPO Cha Mabao 3-0 ilichokipata Ruvu Shooting kutoka kwa Simba SC, katika mchezo uliopigwa uwanja wa Azam Complex, Jijini Dar es salaam Jana May 12,2023 kimeifanya timu hiyo kushuka Daraja hadi Championship kimahesabu.

Mabao ya Simba kwenye mchezo huo yalifungwa na Clatous Chama dakika ya 30 na Pape Sakho aliyefunga mawili dakika ya 72 na 90.

Matokeo hayo yanamaanisha Ruvu Shooting imeipa mkono wa kwa heri Ligi Kuu ya NBC (NBC Premier League 2022/2023) kuelekea mechi mbili za mwisho.

Ruvu Shooting imebakiwa na mechi mbili mkononi ambazo hata ikishinda itafikisha pointi 26 ambazo ni pungufu kwa Mbeya City iliyopo nafasi ya 14 na pointi 27 ikiwa imebakiza mechi tatu tu.

Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

Ruvu Shooting yashuka Daraja 2022/2023

Kwa maana matokeo yeyote itakayoyapata Ruvu katika mechi mbili zilizosalia hayataivusha katika nafasi mbili za mkiani kwa maan ya nafasi ya 16 na 15 hivyo inashuka daraja moja kwa moja.

Ikumbukwe moja ya sheria za Ligi Kuu ni kushuka daraja moja kwa moja kwa timu mbili zitakazomaliza mkiani huku zile zitakazoishia nafasi za 13 na 14 kuamuliwa na mechi za mtoano ‘Play Off’.

Mechi mbili za mwisho za Ruvu itacheza na timu za kanda ya kati kwa maana ya Singida Big Stars iliyojihakikishia kumaliza katika nafasi nne za juu kwenye Msimamo pamoja na Dodoma Jiji inayohaha kutocheza Play Off.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha pointi 67 baada ya kucheza Michezo 28, nyuma ya Mabingwa watetezi, Young Africans wenye pointi 71 baada ya kucheza Michezo 27, ikisalia katika nafasi ya pili, ikiwa imebakiwa na mechi mbili dhidi ya Coastal Union na Polisi Tanzania.

Katika hatua nyingine Klabu ya Young Africans inaweza kutawazwa Mabingwa kwa msimu wa pili mfululizo endapo watashinda mchezo wa leo dhidi ya Dodoma Jiji, kwani itafikisha pointi 74 ambazo haziwezi kufikishwa na Simba anayefuata kwenye nafasi ya Pili hata akishinda mechi zake mbili zilizobaki.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *