LIVE AL AHLY VS WYDAD AC Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 3:00 Usiku. 

SABA wang’oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

Filed in Michezo by on 01/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

SABA wang’oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

SABA wang'oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

SABA wang’oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

WIZARA ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imewasimamisha kazi watumishi saba kutokana na changamoto ya kujirudia kukatika kwa Umeme wakati mechi zikiendelea katika Uwanja wa Taifa wa Benjamin Mkapa uliopo Temeke, Jijini Dar es Salaam.

Uamuzi huo umefikiwa na Waziri wa wizara hiyo, Mheshimiwa Balozi Dkt.Pindi Chana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dkt.Saidi Yakub kupitia taarifa iliyotolewa Aprili 30, 2023 na Eleuteri E.Mangi kutoka Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

“Itakumbukwa 28 Machi, 2023 kulikuwa na mechi baina ya timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda (Uganda the Cranes) kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON). Siku hiyo pia Umeme ulikatika wakati mechi hiyo inaendelea katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.

“Kufuatia hali hiyo, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) alimuelekeza Naibu Waziri Mhe. Hamis Mwinjuma, (Mb) kukaaa na wataalamu kuchunguza tatizo la kukatika Umeme katika Uwanja huo hasa wakati mechi zinaendelea kuchezwa na kupata suluhisho la tatizo hilo.

“Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) alipokea taarifa ya wataalamu wa Umeme ambao walimueleza kuwa chanzo cha hitilafu ya kukatika kwa Umeme Uwanja wa Benjamin Mkapa ni kutokana na mchanganyiko wa Umeme wa Jenereta na Umeme wa gridi ya Taifa katika kuwasha Taa za Uwanja huo na wakapendekeza kuwa Taa hizo ziwashwe na Umeme wa Jenereta pekee.

“Mapendekezo hayo ya wataalam yalitekelezwa kama walivyoshauri. Hata hivyo, hitilafu ya kuzimika kwa Taa imejitokeza tena Usiku wa April 30,2023 wakati ya mechi Nusu Fainali mkondo wa Pili Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika kati ya Yanga na Rivers United ya Nigeria.

“Kutokana na kujirudia kwa hali hiyo licha ya ushauri wa wataalam kufuatwa, Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Balozi Dkt. Pindi Chana, (Mb) ameagiza hatua zifuatazo kuchukuliwa;

SABA wang'oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

SABA wang’oka kukatika Umeme Yanga vs Rivers United

Kusimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wanaohusika na uendeshaji wa uwanja.

Kufuatia agizo hilo na kwa mamlaka aliyonayo, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amewasimamisha kazi watumishi wafuatao ili kupisha uchunguzi,

Aidha, Katibu Mkuu Bw. Saidi Yakubu amewasimamisha kazi ili kupisha uchunguzi watumishi wafuatao ambao nao wanamajukumu ya uendeshaji wa Uwanja wa Benjamin Mkapa.

  • Gordon Nsajigwa Mwangamilo
  • Gabriel Mwasele
  • Yanuaria Imboru
  • Dkt. Christina Luambano

Wakati huo huo, kufuatia hatua zilizochukuliwa, Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Saidi Yakubu amemteua, Bw. Milinde Mahona kuwa Kaimu Meneja wa Uwanja wa Benjamin Mkapa na uteuzi huo
unaanza mara moja kuanzia leo Mei 1,2023.

Aidha Katibu Mkuu atawasiliana na wadau wote husika ili mechi zitakazochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa zichezwe wakati wa Alasiri/Jioni badala ya Usiku katika kipindi ambacho Wizara ianakamilisha taratibu za kupata mzabuni atakayefanya ukarabati mkubwa katika Uwanja huo kabla ya kuanza kwa msimu ujao wa Ligi au Michuano ya Kimataifa.

Pia, kwa mujibu wa taarifa hiyo,ameagiza mamlaka za nje ya Wizara kufanya uchunguzi wa kukatika Umeme katika Uwanja huo na hatua zaidi kuchukua.

“Wizara inaomba radhi mashabiki wa soka nchini hususani wa timu ya Yanga kwa kadhia iliyojitokeza. Wizara inawaahidi Watanzania wote kwamba itaendeea kufanya ukarabati mdogo na mkubwa ili Uwanja wa Benjamin Mkapa uendelee kutoa huduma na burudani stahiki kwa Watanzania pamoja na nchi jirani zinazotumia uwanja huo,”imeongez taarifa hiyo.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *