Nijuze Habari

SABABU kupanda kwa bei za Mafuta na hatua zinazochuliwa na Serikali

Filed in Habari by on 03/08/2022 0 Comments

Miongoni mwa sababu ni ongezeko la uhitaji wa mafuta duniani,na mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.

Nijuze Habari Application

SABABU kupanda kwa bei za Mafuta na hatua zinazochuliwa na SerikaliSABABU kupanda kwa bei za Mafuta na hatua zinazochuliwa na Serikali

Miongoni mwa sababu ni ongezeko la uhitaji wa mafuta duniani,na mgogoro kati ya Urusi na Ukraine.

1.Ongezeko la Uhitaji wa Mafuta baada ya nchi nyingi kuondoa LOCKDOWN kipindi cha Covid19 na kurejeshwa kwa shughuli Mbalimbali za Uzalishaji mali.

2.Mgogoro kati ya Urusi na Ukraine, ambapo Urusi ni mzalishaji nambari mbili wa mafuta Duniani, baada ya mgogoro kuanza mafuta yote yanayotoka Urusi yamezuiwa kuingia katika soko la Dunia.

Kutokana na hizo sababu kuu mbili, Serikali imeamua kutoa ruzuku ya bilioni 100 kwenye mafuta ili kuwapa wananchi unafuu katika bei ya mafuta.

Kwa kushirikiana na TPDC, Serikali ipo kwenye mchakato wa kuongeza vituo zaidi nchini vya kujazia GESI asilia kwenye magari yaliyowekewa mfumo huo, ili kutatua changamoto ya ongezeko la bei ya mafuta.

Hadi sasa zaidi ya Watanzania 300 kwa mwezi wanabadili mfumo na kuingia kwenye GESI asilia.

Bei mpya za Mafuta Tanzania August 2022

EWURA bei mpya za Mafuta Tanzania August 2022BEI ya mafuta nchini Tanzania, imepanda tena mwezi huu August na kuivuka ile ya July 2022 ambapo petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita na Sh179 kwa kila lita ya dizeli huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita kwa Jiji la Dar es Salaam.

Katika taarifa iliyotolewa Jumanne Agosti 02, 2022 na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA), bei ya rejareja Jijini Dar es Salaam itakuwa Sh 3,410 kwa lita moja ya petroli na Sh3,322 kwa dizeli huku mafuta ya taa yakifika Sh3,765.

mafuta pic

Kutokana na bei hiyo mpya ambayo itaanza kutumika kesho, petroli imepanda kwa Sh190 kwa kila lita ambapo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,220 na Sh179 kwa kila lita ya dizeli ambayo mwezi uliopita iliuzwa Sh3,143 huku mafuta ya taa yakipanda kwa Sh323 kwa kila lita ambako mwezi uliopita yaliuzwa Sh3,442.

Ewura imesema bei hizo mpya ambazo zitaanza kutumika Leo Jumatano Agosti 03, 2022 zimejumuisha ruzuku ya Sh100 bilioni iliyotolewa na Serikali vinginevyo, lita ya petroli ngeuzwa Sh3,630 na dizeli Sh3,734 jijini Dar es Salaam.

“Bei za Mafuta katika soko la dunia zimeendelea kuongezeka na kusababisha bei za mafuta katika soko la ndani kuongezeka pia.”

“Ili kupunguza madhara ya ongezeko hilo katika soko la ndani, Serikali imetoa ruzuku ya bilioni 100 kwaajili ya bei za mafuta hapa nchini kwa August 2022. Serikali kwa kutoa ruzuku hiyo, imepunguza bei za bidhaa za mafuta kwa Agosti 2022,” imeeleza taarifa

TAZAMA HAPA CHINI BEI MPYA ZA MAFUTA KWA TANZANIA NZIMA.

EWURA bei mpya za mafuta Tanzania August 2022

telegram Nijuze Habari

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.