Sababu za Ligi Kuu ya NBC kuwa Nafasi ya 5 Afrika 2023

Filed in Michezo by on 22/05/2023 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Sababu za Ligi Kuu ya NBC kuwa Nafasi ya 5 Afrika 2023

Sababu za Ligi Kuu ya NBC kuwa Nafasi ya 5 Afrika 2023

Sababu za Ligi Kuu ya NBC kuwa Nafasi ya 5 Afrika 2023

Ligi Kuu ya Soka Tanzania (NBC Premier League) imetajwa kushika nafasi ya 5 kwa Ubora Afrika na ya 39 kwa Dunia, kwa mujibu wa Shirikisho la Kimataifa la Historia na Takwimu za Mpira wa Miguu (IFFHS).

Katika Kumi Bora Afrika, Tanzania ndio nchi pekee iliyochomoza katika ya nchi za Afrika Mashariki.

Ligi ya Misri inaongoza Afrika ikifuatiwa na Algeria, Morocco na nafasi ya nne ipo Sudan, huku Nafasi ya tano ndipo ilipo Ligi Kuu ya NBC.

Nafasi ya 6 mpaka 10 zinashikwa na Ligi Kuu ya Afrika Kusini, Angola, Tunisia, Nigeria na Zambia.

Aidha Maswali yamekua mengi, Kuna watu wanajiuliza vipi Tanzania tumewazidi Afrika kusini? Na vipi kuhusu Tunisia? Ukweli ni kwamba.

Hiyo Orodha inahusu Ligi Kuu imara/Bora zaidi na Miongoni mwa Vigezo vilivyotumiwa kupata orodha hii ni hivi hapa.

1.Mechi zake zina uratibu mzuri wa Usimamizi maana yake Mchezo una Waamuzi, Kamishna wa Mchezo (MC), Mratibu Mkuu (GC) na Afisa habari (MCO).

2.Ufuatiliwaji wa Ligi hiyo, Yani Watu wa Taifa husika kwa kiasi gani wanaifuatilia Ligi yao ya ndani? Nadhani halina ubishi Tanzania tupo mbele kwenye hili.

3.Matangazo ya Runinga, Ligi ya Tanzania Bara inarusha Matangazo ya Television kwa michezo yake yote kupitia Azam TV.

4.Ufuatiliwaji wa michezo kwenye Television, Mbali na Kurusha mechi zote Mchezo wa Simba na Yanga unafuatiliwa sana kwenye Television (Viewers).

Aidha zipo sababu nyengine lakini hizi ndio Sababu kubwa zaidi zinazoifanya Ligi Kuu ya NBC kuwa namba 5 Afrika 2023.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *