Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal

Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal
Kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu uliopita, Kiungo Mshambuliaji wa Senegal, Pape Osmane Sakho ametajwa kwenye kikosi cha Timu ya Taifa ya Senegal.DROO ya Robo na Nusu Fainali UEFA Champions League 2022/2023
Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Senegal, Khalou Cisse amemtaja kiungo huyo katika kikosi chake ambacho mwishoni mwa wiki ijayo kitacheza dhidi ya Msumbiji katika kusaka nafasi ya kushiriki Fainali za Mataifa ya Afrika ‘AFCON 2023’.

Sakho aitwa timu ya Taifa Senegal
Sakho ambaye ni mfungaji wa goli bora la Afrika mwaka jana anakuwa mchezaji pekee kutoka Afrika kuitwa kwenye kikosi cha Taifa cha Senegal na Aliou Cisse.
Baada ya kumaliza mchezo wa kesho wa Marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Horoya, Sakho atapata ruhusa ya kwenda kujiunga na Simba hao wa Terenga.
Nyota wengine wa kimataifa wa Simba SC walioitwa timu zao Taifa ni:
Henock Inonga (DR Congo), Clatous Chama (Zambia) na Peter Banda (Malawi).
Kwa upande wa Yanga wameitwa Kipa Djigui Diarra (Mali), Khalid Aucho (Uganda), Stephane Aziz Ki (Burkina Faso), Kennedy Musonda (Zambia) na Fiston Kalala Mayele (DRC).
Kutoka Azam FC wameitwa Ali Ahmada (Comoro) na Kenneth Muguna (Kenya).
KMC wameitwa Emmanuel Mvuyekure na Steve Nzigamasabo (Burundi) na Coastal Union ameitwa kipa Justin Ndikumana (Burundi).
Aidha kutoka Singida Big Stars ameitwa Meddie Kagere kikosi cha timu ya Taifa ya Rwanda.
Sakho kutoka Simba SC ya Tanzania anaungana na Wachezaji wengine wanaocheza katika nafasi za Ushambuliaji walioitwa katika kikosi hicho kama Nahodha Sadio Mane kutoka Bayern Munich, Boulaye Dia kutoka Salerntana, Habib Diallo kutoka Strasbourg, Bamba Dieng kutoka Lorient na Iliman Ndiaye kutoka Sheffield United.
Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi cha Senegal upande wa Walinda Lango ni Seny Dieng (Opr), Alfred Gomis (Como) na Mory Diaw (Clermont)
Mabeki: Youssouf Sabaly (Betis Seville), Noah Fadiga (Brest), Kalidou Koulibaly (Chelsea), Formose Mendy (Amiens), Abdoulaye Seck (Maccabi), Moussa Niakhate (Nottingham), Ismail Jakobs (Monaco) na Abdallah Ndour (Sochaux)
Viungo: Gana Gueye (Everton), Nampalys Mendy (Leicester), Pape Gueye (Seville), Pathe Ciss (Vallecano), Pape Matar Sarr (Tottenham) Na Dion Lopy (Reims)
Senegal itacheza dhidi ya Msumbiji mjini Dakar kwenye Uwanja wa Diamniadio Olympic Machi 24, kisha itacheza ugenini mjini Maputo katika Uwanja wa do Zimpeto, Machi 28,2023.
Senegal inaongoza Msimamo wa Kundi L ikiwa na pointi 6, ikifuatiwa na Msumbiji yenye pointi 4, Rwanda ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 1 huku Benin ikiwa mkiani baada ya kupoteza michezo yote hadi sasa.
- MSIMAMO Kundi D CAF Confederation Cup 2022-2023
- MSIMAMO Kundi C CAF Champions League 2022-2023
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
- RATIBA ya Yanga CAF Confederation Cup 2022/2023 hatua ya Makundi
- RATIBA ya Simba CAF Champions League hatua ya Makundi
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.