Nijuze Habari App

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC

Filed in Michezo, New by on 17/06/2023 0 Comments
Share This

JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA


JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA


AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC, Klabu ya Simba umefikia makubaliano ya kuingia mkataba mpya wa miaka miwili wa kutengeneza na kusambaza jezi na Kampuni ya Sandaland Fashion Wear Limited.

Mkataba huo umesainiwa jana Jijini Dar es Salaam baada ya klabu hiyo kumalizana na Kampuni ya Vunja Bei iliyoingia mkataba miaka miwili iliyopita ukiwa na thamani ya Sh 2 Bilioni.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Simba, Ahmed Ally, alisema kuwa, wameamua kuingia mkataba na Sandaland baada ya kuvutiwa na ofa yao iliyokuwa mara mbili na ile iliyopita ya Vunja Bei.

“Tunajivunia kwa kupata mkataba huu ambao utakuwa ni wa kutengeneza na kusambaza jezi za timu zetu. Ilikuwa ngumu kukataa ofa hii ya Sandaland na utakuwa wa miaka miwili na kila msimu itakuwa ni Sh 2 Bilioni, ikiwa na maana kwa miaka miwili klabu inavuna Sh 4 Bilioni,” alisema Ally.

Kulingana na Mkataba huo, Sandaland wamepewa haki ya kuisimamia Simba kwenye matukio yake ya kimichezo ikiwa ni pamoja na kuhamasisha mashabiki kununua jezi na kwenda uwanjani na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Yusuf Omar Yenga aliwaahidi wanachama, Mashabiki na Wapenzi wa Simba kuwa watashuhudia jezi zenye ubora na zitakazopatikana kwa haraka kwani kwa sasa mzigo upo njiani unakuja.

“Tunawaahidi mashabiki kupata jezi zenye ubora na zitakazopatikana kwa wakati kabla hata ya Tamasha ya Simba Day, kwa vile mzigo kwa sasa upo njiani na tumejipanga kuusambaza mapema na kumfikia kila Mwanasimba,” alisema Yenga aliyefafanua kuwa wameanza kupokea oda za mawakala mikoani ili mzigo ukija usambazwe kuwawezesha wanasimba kupata jezi kirahisi popote walipo.

Yenga aliongeza kywa Sandaland ina maduka makubwa mawili ya kuuza jezi Jijini Dar es Salaam ambayo itawarahisisha wanachama, mashabiki na wapenzi wa Simba kupata jezi za msimu ujao kirahisi, huku wale wa mikoani watapata kwa mawakala watakaojiorodhesha na kuweka oda zao kuanzia sasa.

Kwa upande wa CEO, Imani Kajula alisema iuwa Simba haiwezi kuwa timu kubwa Afrika bila kuwa na uwezo wa kifedha, “leo hii tunasimamia sana kwenye eneo hilo. Kwetu hatua ni safari na leo tunapiga hatua kubwa zaidi.”

“Mashabiki walitwambia wanataka tuwe na jezi bora, zifike kwa wakati na zipatikane kila sehemu.”

“Mwanzoni tulikuwa tunapata milioni 400 kwa mwaka kutokana na jezi. Akaja Vunja Bei akatupa bilioni moja kwa mwaka na huyu wa sasa anakuja kutupa bilioni mbili kwa mwaka. Namshukuru sana Sandaland kuwa mdhamini wa jezi kwa msimu wa 2023/24.

Mwenyekiti wa Bodi Salim Abdallah ‘Try Again’ yeye aliwapongeza Sandaland kwa kupata nafasi hii, alisema kuwa Sandaland alijaribu mara ya kwanza hakufanikiwa lakini muda huu amepata. Namshukuru pia VunjaBei kwa udhamini aliotupatia.”

 

MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.

 
 

Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

 

“Tunajipanga kusajili timu yenye ubora na usajili unakwenda vizuri. Simba inakwenda kuondoa unyonge, Simba ijayo.

Baadhi ya wadau wa habari wakizungumzia mkataba wa udhamini wa jezi ambao Simba imeingia na Sandaland The Only One.

Sandaland amrithi Vunjabei Simba SC,Sandaland amrithi Vunjabei Simba,Simba Sc yaingia mkataba wa Sh bil 4 na Sandaland kutengeneza jezi zake,Sandaland yachukua nafasi za Vunjabei Simba Sc,Mrithi Wa Vunjabei Simba ni Sandaland, Thanks you Vunjabei, Welcome Sandaland Simba.

PIA UNAWEZA KUSOMA👇

Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Share This

Tags: , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *