telegram Nijuze Habari

Senegal Mabingwa AFCON 2021

Filed in Michezo by on 07/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

TIMU ya Taifa ya Senegal, imeandika Historia katika medani ya Soka baada ya usiku wa Jana kunyakua Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2021) baada ya kuichapa Timu ya Taifa ya Misri.

Senegal wamebeba Taji la AFCON kwa ushindi wa Penati 4-2 baada ya sare ya bila kufungana kwa dakika zote 120 katika dimba la Paul Biya Jijini Yaoundé nchini Cameroon.

Shujaa wa Simba wa Teranga ni kipa wa Chelsea ya England, Édouard Mendy aliyeokoa mkwaju wa penati wa nne wa Mafarao uliopigwa na Mohanad Lasheen baada ya awali, Mohamed Abdelmonem kugongesha mwamba shuti lake.

Waliofunga penalti za Misri ni Ahmed Mostafa Mohamed Sayed ‘Zizo’ na Marwan Hamdy pekee.

Upande wa Senegal waliofunga ni Kalidou Koulibaly, Abdou-Lakhad Diallo, Cheikh Ahmadou Bamba Mbacke Dieng na Sadio Mane, wakati mkwaju wa Bouna Junior Sarr uliokolewa na kipa Mohamed Abou Gabal ‘Gabaski ‘.

Mapema tu katika dakika ya tatu mchezo, Senegal walipata penalti baada ya Mohamed Abdelmonem kumuangusha kwenye boksi beki mwenzake, Saliou Ciss lakini Gabaski akaokoa mkwaju wa Mane baada ya kupewa maelekezo na Nahodha wake, Mohamed Salah.

Salah na Mane wote wanacheza Liverpool na hilo linakuwa taji la kwanza la AFCON kwa Senegal katika fainali ya tatu baada ya mwaka 2002 na 2019.

Senegal waliingia katika michuano hiyo wakipewa nafasi kubwa ya kutwaa Ubingwa kutokana na kikosi chao kuundwa na wakali wengi wanaotamba Ulaya wakiemo Golikipa Mendy anaekipiga Chelsea, Kalidou koulibaly, Cheikhou Kouyate, Idrisa Gana Gueye, Ismaila Sarr wakiwa chini ya mzawa Aliou Cisse ambae amekipiga na Timu ya Taifa ya Senegal.

Nyota wa Senegal anaekipiga Liverpool, Sadio Mane ameibuka mchezaji bora wa michuano hiyo akihusika katika mabao sita, amefunga matatu na kutoa pasi za mabao tatu lakini pia akifunga penati iliyoamua mechi fainali ya jana.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *