SERIKALI Kujenga Uwanja mpya Arusha
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
SERIKALI Kujenga Uwanja mpya Arusha

SERIKALI Kujenga Uwanja mpya Arusha
SERIKALI Kujenga Uwanja mpya Arusha, Mkoa wa Arusha umepewa dhamana Kubwa ya Kitaifa ya Kujengwa Kiwanja kipya cha Michezo na kufanya Tanzania kuwa na Viwanja vitatu vinavyokidhi Vigezo na mahitaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) ili kuandaa Mashindano ya AFCON 2027 katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Akikagua eneo kitakapojengwa Kiwanja hicho Kata ya Olmoti Jijini Arusha leo Juni 13, 2023, Mkuu wa mkoa huo Bw. John Mongela amesema kuwa Mkoa umepokea mradi huo kwa mikono miwili na watatekeleza azma ya Tanzania kuwa mwenyeji wa Mashindano hayo makubwa barani Afrika.
“Tunamshukuru Rais kwa moyo wake wa uzalendo wa kuwaletea watanzania maendeleo makubwa, Uwanja huu utabadilisha sana sura ya Mkoa wa Arusha na kuiweka kwenye ramani ya Dunia, tutatekeleza maelekezo ya Wizara yetu ya michezo, maelekezo ya TFF, mwongozo wa Mhe. Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu na mamlaka zote. Sisi kama mkoa tutafanya linalowezekana jambo hili lifanikiwe” amesema Bw. Mongela.
Ili kufikia azma ya Tanzania kuwa wenyeji wa AFCON 2027 kwa kushirikiana na nchi za Kenya na Uganda, tayari Kiwanja cha Benjamin Mkapa cha Dar es salaam kimeanza kufanyiwa ukarabati mkubwa pamoja na Kiwanja cha Amani Zanzibar hatua itakayofanya Tanzania kuwa na viwanja vitatu vinavyokidhi ubora kulingana na Sheria na Kanuni za Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) pamoja na mashindano mengine Duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Saidi Yakubu amesema kuwa lengo la ziara hiyo ni kukagua eneo kitakapojengwa kiwanja cha kisasa cha michezo katika Jiji la Arusha ambayo ikiwa ni hatua ya utekelezaji wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Tanzania kuwa mwenyeji wa mashindano ya AFCON 2027.
“Huu ni ukaguzi wa awali wa eneo utakapojengwa Uwanja wa Michezo hapa Arusha, Sisi Wizara tunawaahidi wakazi wa mkoa wa Arusha pamoja na Watanzania kwa Ujumla kuwa tutajenga Kiwanja cha Kisasa chenye uwezo wa kuchukua watu 30,000 ambacho kina uwezo wa kuchezwa mechi za CAF na mechi ambazo zinatambuliwa na FIFA” amesema Bw. Yakubu.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Aidha, ziara hiyo imeshirikisha Uongozi wa mkoa wa Arusha, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF, Bw: Wallance Karia.
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- Ada/makato ya Lipa kwa M-pesa, Lipa kwa Simu
- ADA za LIPA kwa Airtel Mitandao Yote
- TETESI za Usajili NBC Premier League 2023/2024
- YANGA yashika Nafasi ya 9 Simba ya 10 Afrika 2022/2023
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- Ada zaAirtel Money 2022/2023 | Makato mapya ya Airtel Money
- ADA Mpya za Tigo Pesa (Tigo Pesa Tariffs 2022/2023)
- Ada/Makato ya HaloPesa Tanzania, Halopesa Tariffs 2023
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
