Nijuze Habari

Shiboub Aanza Kazi Simba

Filed in New by on 04/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

Klabu ya Simba SC, jana Jumatatu January 03,2022, ilimtambulisha kiungo wake wa zamani raia wa Sudan, Sharaf Eldin Shaiboub Ali mwenye umri wa miaka 27 Visiwani Zanzibar.

Shiboub ambaye msimu wa mwaka 2019–2020 aliitumikia Simba kabla ya kuachana na Klabu hiyo, amerejea tena na tayari yupo Visiwani Zanzibar kuungana na kikosi cha timu hiyo ambayo itashiriki Kombe la Mapinduzi mwaka huu 2022.

Simba imrejesha Shiboub kwaajili ya kumfanyia majaribio kwenye mashindano hayo na iwapo atamridhisha Kocha Pablo Franco Martin, basi Simba watamsajili kwa mara nyingine katika Dirisha Dogo la usajili ambalo lilifunguliwa December 15,2021.

Shiboub amethibitishwa uwepo wake ndani ya Simba pamoja na kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Ivory Coast Moukoro Cheik Tenana ambaye pia atashiriki michuano hiyo ya mapinduzi kama majaribio kabla ya kusajiliwa.

Wachezaji hao tayari wameshaanza mazoezi Visiwani humo kwaajili ya Michuano hiyo.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.