Nijuze Habari

SIMBA kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki Misri

Filed in Michezo by on 26/07/2022 0 Comments

SIMBA kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki MisriKLABU ya Simba SC kesho Jumatano ya July 27,2022 inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa Kirafiki ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa Barani Afrika (CAF).

Nijuze Habari Application

SIMBA kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki Misri

SIMBA kucheza Mechi nyingine ya Kirafiki MisriKLABU ya Simba SC kesho Jumatano ya July 27,2022 inatarajiwa kucheza mchezo mwingine wa Kimataifa wa Kirafiki ikiwa ni muendelezo wa maandalizi ya kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu, Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ na Michuano ya Kimataifa Barani Afrika (CAF).

Simba SC imethibitisha taarifa za kutarajiwa kucheza mchezo huo wa Kirafiki kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, ambapo imekua njia sahihi ya kuwafikishia ujumbe Mashabiki na Wanachama wake.

Taarifa iliyoandikwa kwenye kurasa za mitandao ya kijamii ya Simba SC imeeleza kuwa kesho Jumatano kikosi cha Msimbazi kitacheza dhidi ya Haras El Hodoud.Simba SC vs Haras El Hodoud July 27,2022

Mchezo huo umepangwa kucheza Mjini Cairo, ambapo kikosi cha Simba SC kitalazimika kusafiri kutoka mjini Ismailia kilipoweka kambi ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/2023 hadi Cairo yalipo Makao Makuu ya nchi ya Misri.

“Kesho Jumatano tutakuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya klabu ya Haras El Hodoud ambao utapigwa jijini Cairo” imeeleza taarifa ya Simba SC

Aidha Simba SC, tayari imecheza michezo miwili ya Kirafiki tangu ilipoanza kambi nchini humo wiki mbili mawili zilizopita, mchezo wa kwanza wakicheza dhidi Ismailia FC na kuambulia sare ya bao 1-1 kisha wakacheza dhidi ya Abou Hamad na kufanikiwa kuibuka na ushindi mnono wa mabao 6-0.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.