Nijuze Habari

SIMBA kucheza Mechi tatu za Kirafiki Misri

Filed in Michezo by on 16/07/2022 0 Comments

SIMBA kucheza Mechi tatu za Kirafiki MisriKLABU ya Simba SC jana Ijumaa July 15,2022 ilianza rasmi maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2013 katika Mji wa Ismailia, nchini Misri na leo Jumamosi imeendelea na mazoezi hayo hapo hapo Ismailia, Misri.

Nijuze Habari Application

SIMBA kucheza Mechi tatu za Kirafiki Misri

SIMBA kucheza Mechi tatu za Kirafiki MisriKLABU ya Simba SC jana Ijumaa July 15,2022 ilianza rasmi maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2013 katika Mji wa Ismailia, nchini Misri na leo Jumamosi imeendelea na mazoezi hayo hapo hapo Ismailia, Misri.

Meneja wa Habari na Mawasiliano Ahmed Ally amesema kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kucheza mechi tatu za Kirafiki kipindi ambacho Klabu hiyo itakuwa Misri.

Ahmed amesema Simba itacheza na wenyeji wao Ismailia na timu ya Taifa ya Misri umri chini ya miaka 20 (U20), na timu ya tatu ambayo watacheza nayo itatangazwa hapo baadae.

Wakati huo huo, Ahmed amesema kundi la pili la wachezaji ambao walibaki Jijini Dar es salaam kutokana na sababu mbalimbali, litatua Misri kesho Jumapili kuungana na wenzao.

Ahmed amewataja wachezaji watakaotua Misri kesho kuwa ni Nassoro Kapama, Mosses Phiri, Taddeo Lwanga na Peter Banda.

Pichani hapa chini mazoezi ya siku ya pili nchini Misri.Mazoezi ya Simba SC Misri

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.