Nijuze Habari

SIMBA kuweka Kambi (Pre Season) Misri

Filed in Michezo by on 12/07/2022 0 Comments

Kambi ya Simba SC MisriKIKOSI Simba SC, kinatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi ya July 14,2022 kuelekea nchini Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi (Pre Season) 2022/2023.

Nijuze Habari Application

SIMBA kuweka Kambi (Pre Season) Misri

Kambi ya Simba SC MisriKIKOSI Simba SC, kinatarajiwa kuondoka nchini Alhamisi ya July 14,2022 kuelekea nchini Misri tayari kwa maandalizi ya msimu mpya wa Ligi (Pre Season) 2022/2023.

Wachezaji wote ambao wataitumikia Simba SC msimu ujao 2022/2023 watakuwepo safarini isipokuwa wale ambao watakuwa kwenye majukumu ya timu za taifa ambao watajiunga haraka watakapomaliza jukumu la timu ya Taifa.

Kambi hiyo ya mwezi mmoja itakuwa katika Mji wa Ismailia ambao Simba inaamini utamsaidia Kocha Zoran Maki na wasaidizi wake kukiandaa kikosi vema.

Kambi ya Simba SC MisriSimba SC imedhamiria kufanya makubwa msimu ujao, baada ya kuambulia patupu msimu wa 2021/2022, kwa kupoteza mataji ya Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho ‘ASFC’ yaliyokwenda upande wa Young Africans SC.

Aidha Kikosi kitarejea nchini August 5 kwaajili ya Tamasha la Simba Day na Agosti 13 kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Yanga SC kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC.

Simba SC itaweka Kambi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Misri kwa mara ya Kwanza, baada ya kufanya hivyo katika nchi za Afrika Kusini na Morocco kwa misimu iliyopita.

Katika hatua nyingine, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally amesema kuwa, kesho usajili tutaendelea kwa kushusha mchezaji mkubwa na huo sio usajili wa Afrika bali Dunia itasimama.

 

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

telegram Nijuze Habari

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.