Nijuze Habari

SIMBA Queens yatinga Fainali ya CECAFA 2022

Filed in Michezo by on 25/08/2022 0 Comments

SIMBA Queens yatinga Fainali ya CECAFA 2022TIMU Simba ya Wanawake ya (Simba Queens) imefanikiwa kutinga Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya AS Kigali WFC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Nijuze Habari Application

SIMBA Queens yatinga Fainali ya CECAFA 2022

SIMBA Queens yatinga Fainali ya CECAFA 2022TIMU Simba ya Wanawake ya (Simba Queens) imefanikiwa kutinga Fainali ya Michuano ya Ligi ya Mabingwa Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya AS Kigali WFC katika mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ushindi huo unaipeleka Simba Fainali hiyo na sasa itakutana na SHE Corporates kutoka Uganda katika mchezo wa Fainali utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa Azam Complex.

SIMBA kuzifuata Asante Kotoko na Al Hilal keshoKiungo mkabaji Aquino Corazone ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipatia Simba Queens bao la kwanza dakika ya 14 kabla ya Opa Clement kuongeza la pili kwenye dakika 30 ambapo dakika tisa baadaye Amina Ramadhani akongeza la tatu na kuifanya Simba kwenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao 3-1.

Kipindi cha pili Simba ilirejea mchezoni kwa kasi ile ile ambapo ilifanikiwa kuongeza mengine mawili kupitia kwa Aquino dakika ya 47 na Diana William dakika ya 84.

Simba inaenda kukutana na SHE Corporates ambao walikuwa wote kundi moja, kundi B na Simba iliwafunga mabao 2-0 katika hatua ya makundi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.