Nijuze Habari

Simba waandika barua kwenda Bodi ya Ligi, ishu ya mkataba wa GSM

Filed in Michezo by on 07/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KLABU ya Simba SC imeandikia barua Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) kuhoji juu ya mkataba wa udhamini wa kampuni ya GSM katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara huku pia wakiwa wadhamini wa Klabu ya Young Africans SC.

Katika barua hiyo iliyosainiwa na Mtendaji Mkuu wa Simba SC, klabu hiyo imesema kuwa haifahamu kwa undani juu ya mkataba huo na wao watanufaika vipi zaidi tu ya kufahamishwa kutumia nembo ya GSM kwenye tiketi na jezi zao wakati wa mechi za Ligi hiyo.

Lakini pia Simba imesema GSM kuwa wadhamini wa Ligi Kuu wenza inaleta mgongano wa kimslahi kwa sababu ni wadhamini wa Young Africans pia, klabu ambayo kwa pamoja na mdhamini wao lengo lao ni kutwaa ubingiwa Ligi kama wao Simba SC.

Aidha November 23, 2021 Kampuni ya GSM iliingia mkataba wa Udhamini Mwenza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara (NBC Premier League) kwa dau la Sh. Bilioni 2.1 kwa miaka miwili.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.