Nijuze Habari

Simba Warejea Dar es salaam

Filed in Michezo by on 07/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

KIKOSI cha Simba SC kimerejea salama Jijini Dar es Salaam kwaajili ya maandizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Young Africans SC Jumamosi hii ya December 11,2021 kwenye wa Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Klabu hiyo ilikuwa Zambia tangu Ijumaa ambako walikwenda kwaajili ya mchezo dhidi ya wenyeji Red Arrows, mchezo wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Aidha Simba walifungwa mabao 2-1 kwenye mchezo huo, lakini walifanikiwa kufuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa mabao 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Jijini Dar es Salaam.

Kabla ya kurejea Tanzania, Klabu hiyo jana ilifanya mazoezi Jijini Lusaka, Zambia kwaajili yakuwaweka fiti wachezaji.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.