Nijuze Habari

SIMBA yaitwa Afrika Kusini

Filed in Michezo by on 22/06/2022 0 Comments

Mamelodi Sundowns FCMABINGWA wa Afrika Kusini, Klabu ya Mamelodi Sundowns wamepanga kuialika Simba SC ya Tanzania katika michuano maalum ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.

Nijuze Habari Application

SIMBA yaitwa Afrika Kusini

Mamelodi Sundowns FCMABINGWA wa Afrika Kusini, Klabu ya Mamelodi Sundowns wamepanga kuialika Simba SC ya Tanzania katika michuano maalum ya kujiandaa na msimu mpya wa 2022/2023.

Simba SCMamelodi Sundowns imepanga kuzialika timu tatu kutoka nje ya Afrika Kusini, ambazo zitatoa ushindani wa kweli kwenye michuano hiyo itakayopigwa kwa muda wiki moja tu.

Kwa mujibu wa Meneja mawasiliano wa klabu ya Mamelodi Sundowns, Shupi Nkgadima amesema maandalizi ya michuano hiyo yanakwenda vizuri na wanaamini yatazisaidia timu shiriki kwaajili ya msimu ujao wa 2022/2023.

TP MazembeKlabu nyingine zinazotajwa kuwa kwenye mpango wa kualikwa ni Mabingwa mara tano wa Afrika, TP Mazembe kutoka DR Congo na Al Hilal ya Sudan.

Al Hilal FCSimba SC imewahi kuandaa michuano kama hiyo iliyoitwa (Simba Super Cup) mapema Mwaka 2021 Jijini Dar es salaam, huku timu za TP Mazembe na Al Hilal zikialikwa.

Inatajwa kuwa michuano hiyo inatarajiwa kupigwa kuanzia rasmi July 29,2022.

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.