Nijuze Habari

SIMBA yamgomea Morrison

Filed in Usajili by on 21/06/2022 0 Comments

Bernard Morrison Simba SCUONGOZI wa klabu ya Simba SC umegoma kumpa ‘release letter’ winga Mghana Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 29 mpaka mkataba wake utakapomalizika.

Nijuze Habari Application

SIMBA yamgomea Morrison

Bernard Morrison Simba SCUONGOZI wa klabu ya Simba SC umegoma kumpa ‘release letter’ winga Mghana Bernard Morrison mwenye umri wa miaka 29 mpaka mkataba wake utakapomalizika.

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya uongozi wa Simba ni kuwa Morrison ambaye Simba ilimpa mapumziko, aliuomba uongozi umpatie barua ya kumuacha ili aweze kujiunga na timu nyingine.

Bernard Morrison Simba SCHata hivyo Simba ‘wameweka ngumu’ wakimtaka asubiri mpaka mkataba wake umalizike August 14 mwaka huu, lakini pia Morrison ameambiwa kuwa kama amepata timu, aitaarifu timu hiyo kufuata taratibu za usajili kwani bado yungali na mkataba na Simba SC.

Aidha Kuna taarifa kuwa Morrison huenda akajiunga na Mabingwa wapya wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League 2021/2022) Young Africans SC na anaomba release letter ili ajumuishwe kwenye usajili wa michuano ya CAF na Simba wanafahamu hilo hivo hawana tatizo zaidi ya kusubiri mwisho wa mkataba.

UNAWEZA PIA KUSOMA PIA👇

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.