Nijuze Habari

Simba yamtambulisha Kocha Mpya

Filed in Michezo, Usajili by on 16/11/2021 0 Comments

KLABU ya Simba SC imemtambulisha Mspaniola, Don Daniel De Castro Rayes kuwa kocha wake mpya kwaajili ya mazoezi ya utimamu wa mwili, akichukua nafasi ya Mtunisia, Adel Zrane aliyeondolewa mwezi uliopita.

Nijuze Habari Application

KLABU ya Simba SC imemtambulisha Mspaniola, Don Daniel De Castro Rayes kuwa kocha wake mpya kwaajili ya mazoezi ya utimamu wa mwili, akichukua nafasi ya Mtunisia, Adel Zrane aliyeondolewa mwezi uliopita.

Rayes aliyewahi kufanya kazi Politehnica Las, Rapid Bucharest za Romania na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 18 ys Real Madrid ya kwao nchini Hispania atakuwa chini ya Kocha Mkuu, Mspaniola pia, Pablo Franco Martin aliyewasili Jumanne iliyopita kuchukua nafasi ya Mfaransa, Didier Gomes Da Rosa aliyeondolewa klabuni hapo baada ya kushindwa kutimiza majukumu yake vema.

Soma: Magazeti ya Jumanne November 16,2021

Kocha huyo mwenye Bachelor ya Physical ya Fitness Training aliyosomea katikka Chuo cha Real Madrid anaungana na makocha wengine ambao ni Thierry Hitimana, Suleiman Matola wote wasaidizi na Pablo Franco Martin kocha Mkuu.

Kusajiliwa kwa Kocha huyo kunaifanya Simba SC ibakiwe na pengo la kocha wa makipa ambaye atachuku nafasi ya Mbrazili, Milton Nienov aliyeondolewa sambamba na Gomes na Zrane.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.