Nijuze Habari

SIMBA yamtambulisha kocha wa Viungo na Msaidizi

Filed in Usajili by on 16/07/2022 0 Comments

Zoran Maki Simba SCKLABU ya Simba SC imetangaza kufikia makubaliano na Sbai Karim raia wa Tunisia kuwa Kocha wake Viungo pamoja na Kocha Msaidizi.

Nijuze Habari Application

SIMBA yamtambulisha kocha wa Viungo na Msaidizi

Zoran Maki Simba SCKLABU ya Simba SC imetangaza kufikia makubaliano na Sbai Karim raia wa Tunisia kuwa Kocha wake Viungo pamoja na Kocha Msaidizi.

Katika taarifa yake Simba SC imesema kuwa itakuwa na makocha wasaidizi wawili, ambao ni mzawa Seleman Matola na Sbai Karim kwenye kumsaidia Kocha Mkuu Zoran Maki ili kutimiza majukumu yake ipasavyo.

Sbai Karim Simba SCSbai na Kocha Zoran wanafahamiana vizuri kwani wamefanya kazi pamoja katika Timu za Wydad Casablanca (Morocco), CR Belouzdad (Algeria) Al Hilal (Sudan) na Al Tai (Saudi Arabia) akiwa msaidizi wake.

Sbai ni kocha msomi mwenye leseni ya Daraja A ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Sbai amewahi kuifundisha Klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kuanzia 2017 mpaka 2020 na kufanikiwa kuchukua mataji makubwa ya Afrika.

Msimu wa 2018/2019 alicheza mchezo wa CAF Super Cup lakini timu yake ya Wydad ilipoteza mchezo huo, msimu wa 2020/2021 aliitumikia Klabu ya Al Hilal ya Sudan.

Uongozi wa klabu ya Simba SC unasema kuwa umezingatia uhusiano chanya uliopo baina ya Kocha Zoran na Sbai ambapo Simba inaamini kufahamiana kwao kutarahisisha muunganiko wa haraka kikosini kuelekea msimu mpya wa Ligi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.