Nijuze Habari

SIMBA yamtambulisha rasmi Kocha mpya

Filed in Usajili by on 12/07/2022 0 Comments

Zoran Maki Simba SCKLABU ya Simba SC, imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Zoran Maki mwenye umri wa miaka 58 mbele ya waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine kocha huyo amesema ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na Simba SC kupata mafanikio makubwa kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika.

Nijuze Habari Application

SIMBA yamtambulisha rasmi Kocha mpya

Zoran Maki Simba SCKLABU ya Simba SC, imemtambulisha rasmi Kocha Mkuu, Zoran Maki mwenye umri wa miaka 58 mbele ya waandishi wa habari, ambapo pamoja na mambo mengine kocha huyo amesema ana kazi kubwa ya kufanya kutokana na Simba SC kupata mafanikio makubwa kwenye michuano ya kimataifa barani Afrika.

Baada ya Utambulisho Zoram amesema yupo tayari kwa mchezo wa Deby dhidi ya Young Africans SC, unaotarajiwa kupigwa August 13,2022 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Jijini Dar es salaam.

Miamba hiyo ya Kariakoo inatarajiwa kukutana kwa mara ya kwanza msimu wa 2022/2023 ukiwa ni mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii, ambao pia utatumika kama kiashirio cha kufungua msimu huo mpya wa 2022/2023.

Kocha Zoran amejinasibu kuwa tayari kwa mchezo huo alipojibu swali la Mwandishi wa Habari katika Mkutano Maalum wa Kumtambulisha uliofanywa leo Jumanne July 12,2022 Hoteli ya Serena Jijini Dar es salaam.

CV ya Zoran Manojlović Kocha Mpya wa Simba SC

MSUVA ashinda kesi dhidi ya Wydad Casablanca

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne July 12,202

YANGA yatambulisha beki kutoka Dr Congo

Zoran Maki Simba SCKocha huyo raia wa Serbia amesema kuwa aliwahi kukutana na Joto hilo nchini Angola, Alegria, Morocco na Sudan, hivyo kwake ni jambo la kawaida na wala haofii mchezo dhidi ya Simba SC.

“Nimefundisha Soka Barani Afrika, kwa bahati nzuri kila nilipokwenda nimekutana na changamoto ya Dabi, nilipokua Angola nafundisha klabu Primeiro de Agosto niliwahi kucheza dhidi ya Petro Atlético [Mashabiki 50,000], Nikiwa Morocco na klabu ya Wydad Casablanca nilicheza dhidi ya Raja Casablanca [Mashabiki 70,000], Sudan nilipokua na Al Hilal nilicheza dhidi ya Al Mereikh [Mashabiki 50,000] na Algeria nilipokua na CR Belouizdad nilicheza dhidi ya USM Algiers [Mashabiki 40,000],”

“Hata hapa Tanzania kuna Dabi nzuri sana kati ya Simba SC na Young Africans, hivyo popote utakapofanya kazi unatakiwa kujiandaa na Dabi, kwa hiyo unatakia kuwa na muda mzuri wa maandalizi.” Amesema Kocha Zoran

Kipimo cha kwanza kwa Kocha Zoran akiwa na Simba SC atacheza dhidi ya Young Africa katika mchezo wa kuwania Ngao ya Jamii August 13, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.