Nijuze Habari

SIMBA yanasa saini ya beki Muivory Coast

Filed in Usajili by on 22/07/2022 0 Comments

Mohammed Quattara Simba SC

Nijuze Habari Application

SIMBA yanasa saini ya beki Muivory Coast

Mohammed Quattara Simba SC

KLABU ya Simba SC imetangaza kukamilisha usajili wa Mlinzi wa kati, Mohammed Quattara kutoka Al Hilal ya Sudan kwa mkataba wa miaka miwili, akichukua nafasi ya Pascal Wawa aliyeondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita wa 2021/2022.

Mohammed Quattara Simba SCQuattara mwenye umri wa miaka 23 ambaye ni raia wa Ivory Coast ametua Simba SC kutokea Al Hilal ya Sudan, usajili wake ni miongoni mwa chaguo la Kocha Zoran Maki ambaye wamewahi kufanya kazi pamoja nchini Sudan katika Klabu ya Al Hilal.

Mohammed Quattara Simba SCTayari Ouattara ameshajiunga na kikosi cha Simba SC nchini Misri kinachoendelea na kambi ya maandalizi kwaajili ya msimu ujao wa Mashindano 2022/2023.

Mohammed Ouattara ni mlinzi mwenye uzoefu na soka la Afrika, ambapo pamoja na Al Hilal pia amewahi kucheza Wydad Athletic Club ya Morocco.

Video ya utambulisho ya Ouattara imeonesha akiwa Jangwani akiokota jezi ya klabu ya Simba SC ambayo ataitumikia kwa msimu ujao wa 2022/2023.

 

Ouattara anakuwa Mchezaji wa nne wa kimataifa katika dirisha hili la usajili, akitanguliwa na Moses Phiri wa Zambia, Victor Akpan wa Nigeria na Augustine Okrah wa Ghana, wengine waliosajiliwa kipindi hichi ni wazawa Habib Kyombo na Nassoro Kapama.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.