SIMBA, Yanga zakutana na Rungu la TFF
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
SIMBA, Yanga zakutana na Rungu la TFF
Katika adhabu zilizotolewa ni pamoja na faini ya milioni tano kwa Klabu ya Yanga kwa kosa la kuingia uwanjani kwa kupitia mlango usio rasmi November 5 2023 mchezo dhidi ya Simba SC.
Wakati Yanga wakikutana na adhabu hiyo Simba wao wametozwa milioni moja kwa kosa la wachezaji wake kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia suala hilo lililofanya mchezo huo kuchelewa kuanza kwa muda wa dakika 4 na kuvuruga mpango kwa warusha matangazo Azam TV.
Kibu Dennis aliyefunga bao katika mchezo dhidi ya Yanga ametozwa faini ya laki tano kwa kosa la kushangilia mbele ya jukwaa la mashabiki wa Yanga kwa kuonesha ishara ya kuwafunga mdomo.
Mbali na Kibu pia Henock Inonga ametozwa faini ya laki tano kwa kosa la kushangilia bao mbele ya maofisa wa benchi la ufundi la Yanga sawa na Kocha Msaidizi wa Yanga Moussa Ndao kwa kosa la kuwatolea lugha ya matusi maofisa wa benchi la ufundi la Simba.
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa Djigui Diarra naye ametozwa faini ya laki tano kwa kosa la kwenda kushangilia mbele ya benchi la ufundi la Klabu ya Simba.
Katika hatua nyingine, Kiungo wa Yanga, Khalid Aucho amefungiwa kutocheza michezo mitatu na faini ya Tsh laki tano kutokana na kosa la kumpiga kiwiko mchezaji wa Ibrahim Ajibu wa Coastal Union Novemba 08, 2023 katika Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Katika mchezo huo pia Coastal Klabu ya Coastal Union imetozwa Tsh Millioni moja kwa kosa la wachezaji kuchelewa kutoka nje ya chumba cha kuvalia nguo, jambo lililosababisha mchezo kuchelewa kuanza kupindi cha kwanza na baada ya mapumziko, hivyo kuharibu program za mrusha matangazo ya runinga (Azam TV) ambaye ni mdhamini mwenye haki za matangazo ya runinga.
Mganda huyo atazikosa mechi za Mtibwa Sugar 16 December 2023, Tabora United 22 December na 26 dhidi ya Kagera Sugar.

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
