Nijuze Habari

Simba yapangwa kundi D Kombe la Shirikisho Afrika

Filed in Michezo by on 28/12/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

MABINGWA wa Tanzania, Simba SC wamepangwa Kundi D katika Kombe la Shirikisho Barani Afrika pamoja na RS Berkane ya Morocco wanayochezea Mzambia, Clatous Chama na Mkongo, Tuisila Kisinda.

Timu nyingine kwenye Kundi D ni ASEC Mimosa ya Ivory Coast na US Gendarmerie ya Niger, wakati Kundi A lina Pyramids ya Misri, CS Sfaxien ya Tunisia, Al Ahly Tripoli ya Libya na ZANACO ya Zambia.

Kundi B kuna TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), AS Otohi ya Kongo-Brazzaville, Cotton Sport ya Cameroon na Al Masry ya Misri

Kundi C zipo JS Soura ya Algeria anayaochezea mchezaji mwingine wa zamani wa Simba, Adam Salamba, Al Ittihad ya Libya, Orlando Pirates ya Afrika Kusini na mshindi wa jumla kati ya JS Kabylie ya Algeria na Royal Leopard ya Eswatini.

Royal Leopard iliilaza JS Kabylie 1-0 katika mechi ya kwanza nyumbanii, kabla ya mechi ya marudiano kusogezwa mbele hadi Januari kwa sababu ya COVID 19.

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.