Nijuze Habari

SIMBA yataja thamani ya mkataba wake na M-BET

Filed in Michezo by on 01/08/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

SIMBA yataja thamani ya mkataba wake na M-BET

KLABU ya Simba SC na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya M-Bet zimetangaza Thamani ya Udhamini wa Mkabata wa Miaka Mitano walioingia mwanzoni mwa mwezi July 2022.

Simba SC ilitangaza kuingia Mkataba mpya na Kampuni hiyo, baada ya kumaliza mkataba na Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya SportsPesa mwishoni mwa msimu uliopita wa 2021/2022

Leo Jumatatu August Mosi Simba SC na Kampuni ya Kubashiri hiyo zimeanika wazi thamani ya udhamini huo katika hafla maalum iliyohudhuriwa na Wadau wa Klabu hiyo Kongwe katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na Waandishi wa Habari, jijini Dar es salaam.Thamani ya mkataba wa Simba SC na M-BET Tanzania

Thamani ya mkataba wa Simba na M Bet kama Mdhamini Mkuu ni Bilioni 26.168 ambao utadumu kwa kipindi cha miaka mitano.

Mkurugenzi wa Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amesema kuwa M-Bet ni kampuni nambari moja ya Michezo ya kubashiriki na sasa inashirikiana na Klabu nambari moja Tanzania.

Allen Mushi, amesema kuwa wanaamini kama M-Bet ikishirikiana na Simba itajitangaza ndani na nje ya Tanzania.

Mwaka wa kwanza – Bil 4.670
Mwaka wa pili – Bil 4.925
Mwaka wa tatu – Bil 5.205
Mwaka wa nne – Bil 5.514
Mwaka wa tano – Bil 5.853

Jumla ni Bilioni 26, milioni 168 na Tsh. 5,000.SIMBA yataja thamani ya mkataba wake na M-BET

Naye Meneja wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano, Ahmed Ally amesema kuwa hii pesa iliyotajwa haijahusisha malupulupu mengine ambayo Simba itayapata kutoka MBet.

SIMBA yataja thamani ya mkataba wake na M-BETCEO wa Simba SC, Barbara Gonzalez amesema kuwa Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania.

“Leo ni siku kubwa kwa Simba na M-Bet. Swali kubwa ni kwanini M-Bet. Sababu kubwa ni wameweza kukidhi mahitaji yetu.”

“Kwa ukubwa wa Simba ni lazima kujihusisha na kampuni ambayo inaongoza kwenye biashara ambayo wanafanya. Mkiangalia takwimu M-Bet wanaongoza kwa ukubwa Tanzania.”

“Washirika wote wa Simba kwa sasa wamejitoa kwa Simba tu.”

“Commitment ya M Bet kwa Simba, wana-support vitu vingine vingi nje ya uwanja mfano mzuri ni Simba Day”

“Hii ni mara ya kwanza mdhamini mkubwa anakuwa na Senior team pekee (timu ya Wanaume ya Wakubwa), huko nyuma mdhamini mkuu alikuwa kwa timu zote, kwa hiyo tukiamua kutafuta mdhamini wa Simba Queens, Simba U17 na U20 tuna nafasi hiyo” – CEO Barbara Gonzalez.

SIMBA yataja thamani ya mkataba wake na M-BETMwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah (Try Again) yeye amesema Simba ni waungwana, tunawashukuru wadhamini waliopita, sasa tuko na mdhamini mpya na tunaamini tutafanya kazi kwa karibu.

“Leo ni siku ya kuzungumza fedha. Kampuni kubwa hudhamini klabu kubwa.”

“Tunakaribisha makampuni mengine kufanya nayo kazi sababu hii ni klabu ya watu, wasiogope tuko tayari kufanya nao kazi.”

“M-Bet mlichotaka mtakipata. Pesa ni nyingi hizi, tumieni hii nafasi kutanua biashara yenu kupitia mashabiki wetu.”

“Mimi sijawahi kuona Simba Day kama hii, imeandaliwa ikaandalika, naona kama siku haifiki. Tuje kwa wingi siku hiyo.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Salim Abdallah (Try Again).

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.