SIMBA yazindua Channel ya WhatsApp
JIUNGE NA GROUP LETU LA WHATSAPP HAPA
JIUNGE NA CHANNEL YETU YA TELEGRAM HAPA
AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
SIMBA yazindua Channel ya WhatsApp

SIMBA yazindua Channel ya WhatsApp
KLABU ya Simba imetangaza kuzindua rasmi chaneli ya whatsApp ikiwa klabu ya kwanza kufikia hatua hiyo Leo 14 November 2023.
Akizungumza katika Mkutano na Wanahabari mapema leo, Mtendaji Mkuu wa Simba Imani Kajula alisema kuwa Simba ikiwa klabu yenye wafuasi zaidi kwenye mitandao kijamii kuliko klabu yoyote Tanzania, kupia WhatsApp Wanasimba watakuwa karibu zaidi ya timu yao kwa kupata taarifa muhimu kwa haraka.
“Instagram tuna watu zaidi ya 5.5 milioni, Facebook zaidi ya 1.9 milioni, Twitter zaidi ya 1.5 milioni, YouTube tukiwa na zaidi ya 438k, kwenye app imepakuliwa zaidi ya laki saba na hivi karibuni tumeshinda tuzo ya mashabiki bora.”
“Leo tunazindua Simba Sports Club WhatsApp channel. WhatsApp imepakuliwa na watu Bilioni 2.2 duniani ndio mtandao umepakuliwa zaidi duniani. WhatsApp wenyewe walitufata kuwa timu ya kwanza Afrika Mashariki na Kati kuwa na chaneli hii.”
“Ni timu chache kama Kaizer Chiefs, Al Ahly, Barcelona, Real Madrid na Simba tumejiunga. Katika kuijaribu kabla ya kuzindua ndani ya wiki tumepata wafuasi laki moja. Faida kubwa ni mashabiki kupata taarifa na wadhamini wetu kuonyesha bidhaa zao.”
MKWANJA Mrefu Upo Premierbet Leo, kupata odds za Kibabe Tafadhali Bofya HAPA JISAJILI, BASHIRI Utusue.
Karibu Helabet Upige MKWANJA hadi 300,000, Kujiunga Bofya HAPA, Promo Code ya Bonasi Weka NIJUZE, JISAJILI, Deposit na Utusue.

SIMBA yazindua Channel ya WhatsApp
“Hili ni lingine la kwanza kwa Simba kuwa karibu kwa Wenye Nchi. Simba inataka kuja kuwa timu namba moja Afrika na katika hili moja ya sehemu ya kuboresha ni namna ya kutoa habari.”
“Tunapokuwa na chaneli kama hivi ni sehemu ya Wanasimba na watu wengine kupata taarifa sahihi za klabu. Hii ndio klabu ambayo inafanya vitu vyenye faida na tofauti.”
“Ujio wa Simba WhatsApp Channel unakuja na ajira kwa mtu maalumu kuwa na kazi ya kutoa habari,” alisema Kajula
Kajula pia aligusia mchakato wa kupatikana kocha mpya ambapo amesema mchakato huo uko kwenye hatua za mwisho.
Simba WhatsApp Channel sasa ipo tayari kukusogezea taarifa muhimu kuhusu timu yetu.
Simba WhatsApp Channel. “Simba imekua klabu ya kwanza kwenye ukanda wa Afrika Mashariki na Kati kuwa na chaneli maalum ya WhatsApp ambayo itawapa habari mashabiki na wabia wake. Ikiwa inaingoza kwenye mitandao ya jamii, hii ni hatua kubwa kwani zaidi ya watu 2.7 Bilioni wanataumia WhatsApp hivyo Simba itakuwa karibu zaidi ya mashabiki wake na pia kuwa chanzo kizuri cha kuongeza thamani kwa wadhamini wake na wabia wengine.” alisema Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Imani Kajula.
Bonyeza HAPA Kujiunga na Simba Sports Club WhatsApp #WenyeNchi #NguvuMoja

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.
