telegram Nijuze Habari

Simba yazindua Jezi Mpya

Filed in New by on 03/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

 

KLABU ya Simba wamezindua jezi mpya leo Jumatatu ya January 03, 2022, kuelekea mchezo yao kwenye Michuano ya Mapinduzi Cup 2022.

Jezi hizo zimezinduliwa visiwani Zanzibar na Afisa Habari wa Klabu hiyo Ahmed Ally, na zitatumika katika michuano ya Mapinduzi Cup na Kombe la Azam Sports (ASFC).

Kwa sasa Jezi hizo zinapatikana kwenye maduka yote ya Vunja Bei, ambao Afisa habari huyo amewaomba wanasimba kujipatia jezi hizo mapema.

Akizungumzia uzinduzi huo, Afisa Habari Simba SC, Ahmed Ally amesema; “Tumezindua jezi mpya ambazo tutaanza kuzitumia kwenye michuano ya Mapinduzi hapa Zanzibar, pia tutazitumia kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Mashabiki wanaweza kununua jezi zetu mpya kwaajili ya klabu yao, imekua ni kawaida yetu kufanya jambo hili na wengine wamekua wakituiga…”

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *