telegram Nijuze Habari

Simba yazindua Jezi za Kimataifa

Filed in Michezo by on 10/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

MWENYEKITI wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo (katikati), Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba (C.E.O), Barbara Gonzalez (kushoto) na Meneja wa Habari na Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally (kulia) wakionyesha Jezi ambazo zitatumika kwenye Michuano ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika hatua ya Makundi.

Klabu ya Simba leo Alhamisi February 10, 2022 imezindua rasmi jezi mpya ambazo zitatumika kwenye michuano ya kimataifa ambayo klabu hiyo ipo hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

“Leo tunaonyesha jezi yetu ya michuano ya kimataifa ikiwa na logo ambayo inazingatia mambo yote ya utalii.Jezi zitaanza kuuzwa kesho kwenye maduka ya Vunja Bei na Sandaland The Only One.” amesema CEO Barbara.

“Jambo lolote ambalo lina maslahi kwetu kama Bodi ya Utalii lazima tulipe ushirikiano, lazima tulishangilie.

“Simba inapovaa jezi zimeandikwa Visit Tanzania imekuwa na faida sana. Kuvaa jezi hizo kumehamasisha Watanzania na kumekuwepo na ongezeko la watalii kutoka nje ya nchi.”- Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Jaji Mstaafu Thomas Mihayo

Simba imepangwa Kundi D, ikiwa pamoja na US Gendarmerie ya Niger, RS Berkane ya nchini Morocco na ASES Mimosas ya Ivory Coast.

Klabu hiyo inatarajiwa kucheza mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambao utapigwa Jumapili hii kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam dhidi ya ASES Mimosas ya Ivory Coast.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *