LIVE AL AHLY VS WYDAD AC Download HAPA kutazama LIVE kwenye Simu Yako Leo Saa 3:00 Usiku. 

Spika Job Ndugai Ajiuzulu

Filed in New by on 06/01/2022 0 Comments
Share This
NIJUZE HABARI WHATSAPP GROUP

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA


VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA

Nijuze TV App, Mpira Kiganjani Mwako

Spika wa Bunge la Tanzania Job Ndugai amejiuzulu wadhifa wake leo Alhamisi tarehe 6 Januari 2022.

Kwa mujibu wa barua aliyomuandikia Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema uamuzi huo wa kuachia nafasi hiyo ameufanya kwa hiari.

“Naomba kutoa taarifa kwa umma wa Watanzania kuwa leo Tarehe 06 Januari 2022 nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa bunge la Jamhuri ..” imesema sehemu ya taarifa hiyo nakuongeza;

“Pia nakala yangu hiyo ya kujiuzulu nimewasilisha kwa katibu wa Bunge kwa ajili ya hatua stahiki kwa mujibu wa katiba ya nchi na sheria nyingine” amesema Ndugai kwenye taarifa yake kwa umma.

Ndugai ambaye ni mbunge wa Kongwa amesema anawashukuru wabunge, Rais Samia Suluhu Hassan, Serikali, wananchi wa Jimbo la Kongwa na Watanzania wote kwa ushirikiano waliompa kipindi akiwa Spika

Wito wa kujiuzulu

Hatua hiyo imejiri baada ya kuongezeka kwa shinikizo kutoka kwa viongozi mbali mbali ndani ya chama cha CCM kumtaka ndugai kujiuzulu baada ya majibizano kati yake na rais Samia Suluhu Hassan kuhusu serikali kuchukua mikopo ya maendeleo . Rais Samia tayari ameshajitokeza kusema kwamba kauli za Ndugai huenda zinachochewa na hofu za uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2025 .

Mapema leo Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima amemshauri Spika wa Bunge, Job Ndugai kujiuzulu nafasi hiyo kwa madai kwamba hataweza kuliongoza Bunge kwa sababu wabunge wote watakuwa upande wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Askofu Gwajima ameyasema hayo leo Alhamisi Januari 6, 2022 jijini Dar es Salaam wakati akitoa maoni yake kuhusu kauli ya Spika Ndugai kuhusu mikopo aliyoitoa Desemba 28, 2021 wakati akizungumza kwenye mkutano jijini Dodoma.

Katika mkutano huo, Spika Ndugai alisema kukopa kunaongeza mzigo kwa wananchi na kwamba sasa ni wakati wa kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia tozo mbalimbali zilizoanzishwa bila kutegemea mikopo.

Mbunge wa Jimbo la Mvumi Mkoa wa Dodoma (CCM), Livingstone Lusinde naye pia alikuwa amemtaka Spika wa Bunge Job Ndugai kujiuzulu kabla siku ya leo kuisha.

Akizungumza na gazeti la Mwananchi Lusinde alisema anamtaka Ndugai kuchukua hatua hiyo baada ya kujiridhisha kwa kupitia video nzima ya hotuba ya Spika Ndugai aliyoitoa hivi karibuni kwenye mkutano wa Wagogo wa Kikundi kinachofahamika kama Wanyausi.

“Napenda kusisitiza hilo na namtaka leoleo kabla ya siku kuisha awe amejiuzulu kwasababu haiwezekani mtu unaomba msamaha kwa kujitetea.. msamaha hauombwi hivyo kwa kuanza kukanusha kosa ilibidi aongee maneno machache tu” gazeti hilo limemnukuu mbunge huyo .

Ndugai kuomba msamaha

Baada ya ya matamshi yake kuzua mjadala nchini humo Ndugai alijitokeza katika kikao na waandishi wa habari kuomba msamaha kwa ‘rais na Watanzania’ lakini hatua yake hiyo haikutuliza mambo .

Akizungumza na waandishi wa habari Jumatatu Januari 3, 2021 jijini Dodoma, Job Ndugai alisema katika hotuba yake aliyoitoa hivi karibuni hakukuwa na jambo la kukashifu wala kudharau juhudi za Serikali ila alikuwa anasisitiza ulipaji wa kodi na tozo mbalimbali.

Bwana Ndugai alisema kwamba mwishoni mwa mwaka uliopita alikuwa mgonjwa sana hivyo hakuweza kuwa katika nafasi ya kujitetea kwa kile kilichokuwa kinasambaa mtandaoni.

“Hali yangu ya kiafya ilikuwa si nzuri mpaka sasa mnashuhudia sauti yangu ila nataka kuweka sawa kuwa tarehe 26, mwezi Desemba nilialikwa na kikundi kimoja cha watu wa dodoma, wanaoangazia maisha ya wenyeji, kikundi hicho lengo ni ushikamano na kujenga makumbusho ya utamaduni wa watu.

Na hakukuwa kukashifu, Hapakuwa na lolote la kukashifu au kudharau juhudi zozote za serikali, katika mazungumzo yetu zaidi nilisisitiza umuhimu wa tozo na kodi.”

Aliongeza kusema kuwa kama kuna mtu angeona video nzima ya kile alichozungumza, hakuna migongano ambayo ingeweza kutokea;

“Katika mazungumzo yale, baadhi ya watu wakakatakata clip ya video, wakawasilisha ujumbe nusu, ujumbe nusu ule umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, ambao mjadala umesababisha usumbufu wa hapa na pale” amesema Ndugai na kuongeza

“Hapakuwa na lolote la kukashifu wala kudharau juhudi zozote za Serikali, tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono.

Katika mazunguzo hayo ambayo yalienda na video hiyo fupi, ninakiri kuwa mitandao ina nguvu sana na ina uwezo wa kutengeneza agenda.

Binafsi nimeumia sana kwa kauli yangu kuonekana kuwa ninapinga mkopo, mimi binafsi nina ushuhuda wa fedha hizo kutumika kujenga shule nzuri ya kiwango katika jimbo langu.’ alisema wakati huo.

Jibu la rais Samia

Rais wa Tanzania Samia Hassan siku iliyofuata ya tarehe 4 Januari alielezea anachofikiria kilichosababisha kauli zinazoonekana kupinga hatua ya serikali kuchukua mikopo ya kufanya maendeleo.

Katika hotuba yake wakati wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya Uviko-19, rais Samia alisema kauli hizo zinahusiana na azma ya baadhi ya viongozi kutaka kugombea kiti cha urais mwaka wa 2025 .

Bila kutaja jina la kiongozi yeyote rais Samia alielezea kuhusu jinsi alivyowahi kupokea ushauri kwamba ‘atakayempa changamoto serikalini’ sio mpinzani bali ‘kijani mwenzako’ akimaanisha mtu kutoka chama tawala cha CCM .

th

CHANZO CHA PICHA,IKULU

‘Nisengeshangaa kama ni adui yangu ndiye kapiga kelele..aliniambia mpinzani atakutazama unafanya nini ukimaliza hoja zao hawana maneno lakini shati kijani mwenzio anayetizama mbele mwaka wa 2025…2030 huyu ndiye atakayekusumbua’ rais Samia alisema

Rais Samia pia alieleza kilichojiri wakati akichukua madaraka akiongeza ;

“Lakini jengine ni kwamba wakati mmenikabidhi huu mzigo nilianza kusikia lugha zinasema serikali ya mpito, serikali ya mpito, bungeni huko kwa kina Kassim nikarudi katika katiba nikaenda kuangalia serikali ya mpito imeandikwa wapi kwenye katiba, ikitokea nini kunakuwa na serikali ya mpito, sikuona’

Aliendelea kusema;

“Mtu na akili yake anasimama na anahoji kuhusu mikopo na tozo, sio lolote ni homa ya 2025, kwa mtu ambaye nilimtegemea kushirikiana naye kwenye maendeleo, sikutegemea kama angesimama na kusema maneno hayo.

Kwasababu huwezi kuamini mtu mzima na akili yako unaenda kuhoji tozo na mkopo wa 1.3 trilioni kama ndio kwanza imetokea Tanzania, ni uhuru wake kusema chochote lakini ni mtu mnayemtegemea, mnategemea labda atakuwa na uelewa hasa kwasababu mabajeti yote, mikopo yote taarifa za kiuchumi ni ndani ya nyumba yake ndo zinapita, lakini ni homa ya 2025″ alisema rais Samia

Credit: BBC

Download App ya Nijuze Habari Playstore tukutumie Habari zote kwenye Simu yako BILA MALIPO BOFYA HAPA.

Download App ya Nijuze TV Utazame mechi zote kwenye Simu yako BOFYA HAPA

Share This

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *