Nijuze Habari

TAARIFA mpya 4 kutoka Young Africans SC July 26,2022

Filed in Michezo by on 26/07/2022 0 Comments

Yanga kusaini mkataba mpya na SportpesaKLABU ya Yanga SC imebainisha kuwa itasaini mkataba mkubwa wa Kihistoria wa udhamini na Kampuni ya Sportpesa baada ule wa awali kufikia tamati.

Nijuze Habari Application

TAARIFA mpya 4 kutoka Young Africans SC July 26,2022

Yanga kusaini mkataba mpya na SportpesaKLABU ya Yanga SC imebainisha kuwa itasaini mkataba mkubwa wa Kihistoria wa udhamini na Kampuni ya Sportpesa baada ule wa awali kufikia tamati.

Kambi ya Yanga SC AVIC Town KigamboniKIKOSI cha Yanga SC, Leo Jumanne ya July 26,2022 kimeingia siku ya nne katika maandalizi ya kuelekea tukio kubwa la Wiki ya Mwananchi pamoja na msimu mpya wa mashindano wa 2022/2023.

Kambi ya Yanga SC AVIC Town KigamboniTakribani wachezaji 17 tayari wameripoti kambini kuendelea na mazoezi ambapo Beki Yannick Bangala na Kiungo Bernard Morrison wao wanatarajiwa kuwasili Leo Jumanne.

MAGAZETI ya Tanzania Leo Jumanne July 26,2022
Fiston Kalala Mayele Yanga SCTaarifa njema zaidi kwa Wanayanga ni kuwa Mshambuliaji wao, Fiston Kalala Mayele amerejea nchini akitokea DR Congo alipokuwa kwa mapumziko mafupi.

Mayele alitua nchini jana Jumatatu July 25,2022 majira ya saa 12 jioni na moja kwa moja kuelekea Avic Town kuungana na Wachezaji wenzake kwaajili ya maandalizi ya msimu ujao wa 2022/2023.

Mohammed Nasreddine Nabi Yanga SCAidha Kocha Mkuu wa Yanga SC, Mohammed Nasreddine Nabi Leo Jumanne July 26,2022 amekabidhiwa Tuzo ya Kocha Bora wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2021/2022.

Nabi aliingoza Yanga SC kutwaa mataji matatu ambayo ni Ngao ya Jamii, Ligi Kuu ya NBC na kombe la Shirikisho la Azam (ASFC) Msimu uliopita wa 2021/2022, ambapo alishinda mataji hayo yote pasipo kupoteza mchezo hata mmoja.Mazoezi ya Yanga SC AVIC Town Kigamboni

telegram Nijuze Habari

Tags: , , , , , , , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.