telegram Nijuze Habari

TAARIFA Mpya kutoka Yanga SC, March 16,2022

Filed in Michezo by on 16/03/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

TAARIFA Mpya kutoka Yanga SC, March 16,2022

Ratiba ya NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, Ratiba ya Tanzania Bara, NBC Premier League, Ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara, NBC Premier League, Yanga SC, Young Africans SC vs Somalia, Young Africans Sports Club, Jangwani Dar es salaam, Somalia vs Yanga, Somalia vs Young Africans SC, Mechi ya Kirafiki, Mchezo wa Kirafiki.

KLABU ya Young Africans SC imetangaza kuandaa matukio maalum kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Premier League) dhidi ya KMC FC, Mchezo ambao utapigwa Jumamosi ya March 19,2022 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam.

Msemaji wa Klabu hiyo, Haji Sunday Manara amesema kuwa tukio la kwanza litafanyika siku ya kesho Alhamisi Hospitali ya Ocean Road Jijini Dar es salaam katika kumbukumbu ya Mwaka mmoja ya kifo cha aliyekuwa Rais wa Tanzania awamu ya tano, Hayati Dk John Magufuli ambaye alifariki March 17,2021.

Viongozi wa Young Africans chini ya Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, GSM Foundation, benchi la ufundi na wachezaji kadhaa watashiriki kutoa misaada mbalimbali.

Ijumaa Wananchi watakuwa na tukio la kuchangia damu Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama sehemu ya kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan.

Watu 200 wa kwanza katika zoezi hilo watapatiwa jezi mpya za klabu ya Young Africans ambapo Manara amesema hata kama sio mwana Yanga utapatiwa jezi ukiwa miongoni mwa watu hao.

Zoezi hili litafanyika kote nchini ambapo Manara amewataka viongozi wa Matawi ya Yanga kufanikisha matukio ya Uchangiaji damu katika mikoa yao.

Siku ya Jumamosi maadhimisho ya mwaka mmoja wa Rais Samia, Wanayanga watafanya usafi katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea Uwanja wa Benjamin Mkapa kushuhudia Mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya KMC FC.

Klabu hiyo imemuomba Rais Samia awe mgeni wa heshima katika mchezo huo utakaopigwa kuanzia saa moja usiku.

Aidha, siku hiyo kutakuwa na burudani za aina mbalimbali kabla ya mchezo huo ikiwa ni pamoja na Mchezo wa Utangulizi kati ya viongozi wa Yanga dhidi ya Wasanii.

Klabu hiyo pia imesema kuwa Kwenye mchezo wa hisani wa Ali Kimara Rare Diseases Foundation dhidi ya Somalia imetengeneza Shilingi Millioni 41 kupitia mapato yaliyopatikana kwenye mchezo huo na michango iliyotolewa na Viongozi, Mashirika Pamoja na Watu mbalimbali.

Klabu hiyo pia imesema kuwa kwenye mchezo wa hisani wa Ali Kimara Rare Diseases Foundation inawashukuru sana Serikali kupitia Wizara husika, TFF kama wenye mpira wao na vyombo vyote vya habari pamoja na Wanachi waliojitokeza na waliotizama kupitia TV.

MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *