Nijuze Habari

Tanzania yashuka Viwango vya FIFA

Filed in Michezo by on 20/11/2021 0 Comments
Nijuze Habari Application

TANZANIA imeshuka nafasi moja kutoka 130 hadi 131 katika viwango vya ubora wa soka vilivyotolewa na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu, FIFA hapo jana.

Kufanya vibaya kwa Tanzania kwenye michezo miwili ya mwisho ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ilipofungwa mabao 3-0 na sare ya bao 1-1 dhidi ya Madagascar ndicho kisababishi cha kuporomoka kwa Stars.

Tanzania ilishindwa kufuzu na kuishia hatua ya makundi kwenye Kundi J, ikimaliza kwa kushika nafasi ya tatu ikiwa pointi nane, huku kinara DRC ikisonga mbele hatua ya mtoano kwa pointi 11.

Nafasi ya pili ilishikiliwa na Benin iliyokuwa na pointi 10 na Madagscar ilikuwa ya mwisho kwa pointi nne.

Aidha, kwa upande wa Afrika Mashariki Uganda bado wanaongoza wakishika nafasi ya 82, wakifuatiwa na Kenya nafasi ya 102, Sudan 124, Ethiopia 135 na Burundi 140.

Kwa upande wa Afrika Senegal, Morocco, Tunisia, Algeria, Nigeria, Misri na Cameroon zipo katika 50 bora.

Kidunia, Ubelgiji ndio inaongoza ikifuatiwa na Brazil, Ufaransa, England, Argentina, Italia, Ureno, Denmark na Uholanzi.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.