telegram Nijuze Habari

TANZIA: Ally Sonso afarikia Dunia

Filed in Michezo by on 11/02/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application
BEKI wa zamani wa Vilabu vya Lipuli FC, Young Africans, Kagera Sugar FC, Ruvu Shooting FC na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Ally Abdulkarim Mtoni ‘Sonso’ amefariki Dunia leo katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Mtoni alisajiliwa na Young Africans akitokea Lipuli FC ya Iringa msimu wa 2019-2020 kabla ya kuachwa na msimu uliofuata akasajiliwa na Kagera Sugar ambako aliicheza hadi msimu huu alipojiunga na Ruvu Shooting FC.
Aidha Sonso alikuwemo kwenye kikosi cha Taifa Stars kilichoshiriki Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Misri mwaka 2019.
Mungu ampumzishe kwa amani marehemu Ally Mtoni Sonso🙏🙏🙏.
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *