TANZIA: Bernard Membe afariki Dunia

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


TANZIA: Bernard Membe afariki Dunia

TANZIA: Bernard Membe afariki Dunia
Aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bernard Kamilius Membe, amefariki dunia leo asubuhi Ijumaa Mei 12, 2023 akiwa katika Hospitali ya Kairuki Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha hospitali ya Kairuki, Arafa Juba amethibitishia Mwananchi taarifa za kutokea kwa kifo hicho akieleza kuwa kimetokea saa mbili asubuhi.
“Ni kweli Membe aliletwa asubuhi hapa akapatiwa matibabu na wataalam kama ilivyo kawaida mgonjwa anapokuja hospitali, lakini Mungu alimpenda zaidi akafariki saa mbili asubuhi,” amesema Arafa.
Kuhusu ugonjwa uliokuwa unamsumbua, Arafa amesema ugonjwa ni siri ya mgonjwa na daktari hivyo undani wa hilo unaweza kutolewa na familia na si hospitali.
Katika hatua nyingine, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa salamu za rambirambi kwa familia kutokana na msiba huo kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.
“Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Ndugu Bernard Membe. Kwa zaidi ya miaka 40, Ndugu Membe alikuwa mtumishi mahiri wa umma, mwanadiplomasia, Mbunge na Waziri aliyeitumikia nchi yetu kwa weledi. Pole kwa familia, ndugu, jamaa & marafiki. Mungu amweke mahali pema. Amina.”
PIA UNAWEZA KUSOMA👇
- FAHAMU kuhusu Azam Pesa pamoja na Makato yake
- Ada mpya za M-Pesa 2023/2024 | Makato mapya ya M-Pesa
- DOWNLOAD | NYIMBO ZA TENZI ZA ROHONI SWAHILI MIX
- Ada za M-Pesa Songesha 2022/2023
- FAHAMU Jinsi ya Kufungua Akaunti ya M-Koba Vodacom
- MFUMO wa maombi ya Kitambulisho cha Taifa (NIDA) Online
- JINSI ya kupata mikopo ya vijana na wanawake
- Namna ya Kujisajili na Premier Bet Ushinde Mamilioni
- RATIBA kamili NBC Premier League msimu wa 2022/2023
- DOWNLOAD NIDA number | Kitambulisho cha Taifa
- MSIMAMO Ligi Kuu Tanzania Bara 2022/2023
- WAFUNGAJI Wanaoongoza kwa Ufungaji Ligi Kuu
Nijuze TV ni App ambayo ukiwa nayo utaweza kutazama mechi za Ligi Kuu Tz Bara (NBC PREMIER LEAGUE) EPL, WORLD CUP, EPL, LALIGA, SERIA, LIGUE 1, BUNDESLIGA na Ligi nyingine nyingi.