Nijuze Habari

TANZIA: Mzee Mrema afariki Dunia

Filed in Habari by on 21/08/2022 0 Comments

TANZIA: Mzee Mrema afarikiaMWENYEKITI wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema umri wa miaka 77 amefariki Dunia Leo Jumapili, August 21, 2022, asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam.

Nijuze Habari Application

TANZIA: Mzee Mrema afariki Dunia

TANZIA: Mzee Mrema afarikiaMWENYEKITI wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema umri wa miaka 77 amefariki Dunia Leo Jumapili, August 21, 2022, asubuhi, katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Jijini Dar es Salaam.

Mrema aliyewahi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani, alizaliwa December 31,1944, Vunjo huko mkoani Kilimanjaro.

Msemaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili , Aminieli Eligaisha amesema, Mrema alilazwa Hospitalini hapo kuanzia August 16,2022 na kufikwa na umauti huo asubuhi ya Leo.

Enzi za uhai wake, Mwanasiasa huyo aliwahi kuwa Mgombea Urais kupitia NCCR-Mageuzi Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995 baada ya kujiunga na Chama hicho akitokea Chama cha Mapinduzi (CCM).

Mrema aliwahi kuwa Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), Temeke (NCCR Mageuzi) na Vunjo kupitia TLP na hadi anafikwa na umauti alikuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.