Nijuze Habari

TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa wazi

Filed in Michezo by on 03/06/2022 0 Comments

TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa wazi.KLABU ya Young Africans kupitia Mwenyekiti wake wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Ally Mchungahela imetangaza tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo ambayo ni July 10, 2022.

Nijuze Habari Application

TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa wazi

TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa wazi.KLABU ya Young Africans kupitia Mwenyekiti wake wa Kamati ya Uchaguzi Malangwe Ally Mchungahela imetangaza tarehe rasmi ya Uchaguzi Mkuu wa Klabu hiyo ambayo ni July 10, 2022.

Mchungahela amesema Uchaguzi Mkuu utahusisha nafasi za Rais wa timu, Makamu wa Rais na Wajumbe Watano (5).

Na mchakato wa uchaguzi huo unaanza mara moja ambapo June 5 hadi 9, 2022 zoezi la kuchukua fomu linafunguliwa rasmi likifuatiwa na zoezi la mchujo wa wagombea litakalofanywa kuanzia June 10 hadi 11, 2022 likitekelezwa na Kamati ya Uchaguzi ya Klabu hiyo.

Michakato mingine itaendelea huku ratiba kamili ya michakato hiyo hadi kufikia tarehe rasmi ya zoezi la Uchaguzi Mkuu inatarajiwa kubandikwa katika mbao za matangazo Makao Makuu ya Klabu hiyo.

Lakini pia Mchungahela ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ameongeza muda wa wiki mbili kwa matawi yote ya Klabu hiyo nchini Kukamilisha zoezi la Uchaguzi wa Viongozi kwa ngazi zao.

TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa waziKisha nyaraka za Muhtasari na maazimio ya chaguzi hizo ikiwemo Viongozi waliochaguliwa ziwasilishwe Ofisini kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu hiyo Senzo Mbatha Mazingiza.

Mwenyekiti huyo ameyakumbusha matawi yote kuwa viongozi wanaotakiwa kuchaguliwa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu, Mweka Hazina na Wajumbe Watano lakini pia wachaguliwe Wajumbe wengine Wawili ambao watawakilisha Matawi katika Uchaguzi Mkuu wa July 10, 2022.

Gharama ya kuchukua fomu kwa anayegombea nafasi ya Rais wa klabu na Makamu wa Rais ni Tsh 200,000 kila mmoja, huku wajumbe ikiwa ni Tsh 100,000.

Zoezi hilo likikamilika Young Africans SC itakuwa na Rais wa kwanza kwenye historia, na inakuwa imehama rasmi kwenye mfumo wa zamani.TAREHE rasmi ya uchaguzi Mkuu Yanga yawekwa wazi

UNAWEZA PIA KUSOMA๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡๐Ÿ‘‡

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags:

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.