Tetemeko la Aridhi Singida na Dodoma

AJIRA MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA
AUDIOS MPYA ZA WIKI BONYEZA HAPA
VIDEOS MPYA ZA WIKI HII BONYEZA HAPA


Tetemeko la Aridhi Singida na Dodoma

Tetemeko la Aridhi Singida na Dodoma
Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 4.9 na 4.3 katika kipimo cha richter limetokea kwenye Mikoa ya Singida na Dodoma leo February 17, 2023.
Akithibitisha taarifa hizo Mjiolojia Mwandamizi kutoka Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Gabriel Mbogoni amesema kuanzia jana yametokea matetemeko ya ardhi matatu nchini Tanzania.
Read this: WAFUNGAJI wanaoongoza kwa magoli Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara
Mbogoni amesema kuwa moja lilitokea maeneo ya mpaka wa Singida na Dodoma likiwa na ukubwa wa 4.9 katika kipimo cha richter, jingine lilitokea asubuhi ya leo likiwa na ukubwa wa 4.3 likifuatiwa na lenye ukubwa wa 4.9 na haya mawili yametokea katika wilaya ya Manyoni.
Hata hivyo Mbogoni amesema mpaka sasa hakuna taarifa zozote za madhara ambayo yamesababishwa na matetemeko ya ardhi ambayo yametokea jana Alhamisi na leo Ijumaa.
Ikumbukwe kwamba mikoa ya Singida na Dodoma imepitiwa na Ukanda wa Bonde la Ufa la Afrika Mashariki mkondo wa Mashariki.
Maeneo ya ukanda wa Bonde la Ufa kwa kawaida ni maeneo tete ya mabadiliko ya kijiolojia ambayo hukumbwa na matetemeko ya ardhi na milipuko ya Volkano.