Nijuze Habari

Tetesi na Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara

Filed in Usajili by on 03/01/2022 0 Comments
Nijuze Habari Application

KIUNGO wa zamani wa klabu ya Simba SC James Kotei raia wa Ghana amejiunga na klabu ya DTB FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) kwa mkataba wa mwaka mmoja.

Beki wa kushoto wa zamani wa Singida United, Shafiq Batambuze raia wa Uganda amejiunga na klabu ya DTB FC inayoshiriki ligi daraja la kwanza (Championship) kwa mkataba wa miezi sita akitokea klabu ya Kabwe Warriors ya Zambia.

 

Kiungo wa zamani wa Simba Sharaf Eldin Shaiboub Ali na winga, Moukoro Cheik Tenena kutoka Ivory Coast wapo Visiwani Zanzibar na kikosi cha Mabingwa hao kwaajili ya majaribio katika michuano ya Mapinduzi.

Wachezaji hao wakifanikiwa kulishawishi benchi la ufundi la Simba SC watasajiliwa moja kwa moja katika dirisha hili dogo la Usajili Ligi Kuu Tanzania Bara.

Winga wa kimataifa wa Nigeria anayecheza klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco Michael Babatunde mwenye umri wa miaka 29 anatajwa kuwa kwenye hatua za mwisho kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Simba SC.

Kiungo wa Akwa United FC, Udoh Etop David raia wa Nigeria yupo nchini kwaajili ya majaribio ya kujiunga na klabu ya Simba SC.

Udoh mwenye umri wa miaka 22 anatajiwa kushiriki Mashindano ya Mapinduzi Cup yanayofanyika Visiwani Zanzibar.

Kiungo wa zamani wa Simba SC, Gerson Fraga raia wa Brazil anatarajia kuwasili nchini kwaajili ya kujiunga na Simba SC.

Klabu ya Simba SC ina mpango wa kumsajili Winga Harrison Mwenda raia wa Kenya kutoka Kabwe Warriors ya Zambia.

Aliyekuwa Mlinda mlango wa Klabu ya Young Africans SC, Ramadhan Kabwili huwenda akajiunga na Klabu ya Mbeya City FC.

Klabu ya Simba SC na RS Berkane zimefikia makubaliano ya kumrejesha nchini Tanzania Clatous Chama, na kilichobaki na Simba kulipa nusu ya kiasi walichopokea wakati wa kuumuza Chama Ili Klabu hiyo ya Morocco imwachie Mwamba wa Lusaka.

telegram Nijuze Habari
MSIMAMO NBC PREMIER LEAGUE 2022/2023

Tags: , ,

About the Author ()

Leave a Reply

Your email address will not be published.